CCM YAJIPANGA KUWAFUKUZA WAKINA LUGOLA,MWAMBALASWA,MURAD,NI WALE WABUNGE WENYE KASHFA YA RUSHWA,SOMA HAPO KUJUA
![]() |
| Mh.Kangi Lugola, Mbunge wa Mwibala (Wakwanza), Mh.Sadiq Murad, Mbunge wa Mvomero pamoja na Mh.Victor Mwambalaswa, Mbunge wa Lupa |
CHAMA Cha
Mapinduzi (CCM) kimeanza harakati za kuwatema makada wake wanaotuhumiwa
kujihusisha na vitendo vya rushwa kwa madai ya kuonesha taswira hasi kwa
wananchi, anaandika Moses Mseti.
Shaka Hamudu Shaka, Katibu Mkuu wa Umoja wa
Vijana wa CCM-Taifa (UVCCM) amesema kuwa, wabunge wa chama hicho wanaotuhumiwa
pia wengine wanaojihusisha na vitendo vya rushwa wanapaswa kutimliwa ndani ya
chama hicho.
Kauli ya Shaka inakuja ikiwa ni siku chache baada ya wabunge
wanne wa CCM kupandishwa kizimbani wakituhumiwa kuomba rushwa ya Sh. 30 milioni
kutoka kwa Mbwana Magotta, Mkurugenzi wa Halmashauli ya Gairo.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)
imewapandisha kizimbani Kangi Lugola, Mbune wa Mwibara; Ahmed Sadiki, Mbunge wa
Mvomelo; Victor Mwambalaswa, Mbunge wa Lupa na Richard Ndasa, Mbune wa Sumve
kutokana na tuhuma hizo.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara jana, uliofanyika katika
Uwanja wa Magomeni, Kata ya Kirumba Wilaya ya Ilemela, mwanza, Shaka amesema
kuwa wabunge na watumishi wa umma wanaojihusisha na rushwa wanapaswa kuchukulia
hatua.
Shaka amesema
kuwa wabunge wa chama hicho tawala wanaotuhumiwa kuomba na kupokea rushwa,
wanapaswa kuchukuliwa hatua ikiwemo kuvuliwa madaraka na pia isiishie
kupandishwa kizimbani pekee.
“Wabunge ambao wameshindwa kuwatumikia wananchi waliowapa ridhaa
hiyo na wameanza kupokea rushwa wanapaswa kutokuonewa aibu, inapaswa
wachukuliwe hatua zaidi ya kupelekwa mahakamani ili iwe fundisho kwa wengine.
“Tunapaswa kuheshimu sheria za nchi na Katiba ya nchi yetu, mtu
ambaye atabainika kujihusisha na kuvunja sheria anapaswa kuchukuliwa hatua, sisi ndani
ya chama chetu (CCM) hatuungi mkono wabunge wanaojihusisha na rushwa,” amesema
Shaka.
Licha ya kutowataja kwa majina Shaka aliwagusa wabunge hao
kwenye maelezo yake kwa kuwa ndio waliopandishwa kizimbani kuanzia Aprili 1
mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Miraj Mtaturu, Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza ameunga mkono kauli
ya Shaka “CCm hatuungi mkono wabunge ambao wanapokea rushwa, viongozi wote
wanaojihusisha na vitendo hivyo wanapaswa kuchukuliwa hatua, wao wanapaswa
kuwatumikia Watanzania na sio kuomba rushwa
Habari hii kwahisania ya Mwanahalisi oline

No comments
Post a Comment