WASOMI WAANZA MCHOKA RAIS MAGUFULI,DK LWAITAMA AMRUSHIA KOMBORA,SOMA HAPO KUJUA
![]() |
| John Magufuli, Rais wa Tanzania |
RAIS John Magufuli anatajwa kuwa ni rais mchochezi
na anayefanya mambo yake ili kuonesha anaendesha mapambano dhidi ya wapinzani
wake, anaandika Happyness Lidwino.
Dk. Azaveli Lwaitama, Mhadhiri
Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema, yapo baadhi ya mambo ambayo
Rais Magufuli amekuwa akiyafanya ili kukomoa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba
ya Wananchi (Ukawa).
“Mfano
siku aliyoteuliwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliongea kauli
tata akaendelea na kauli hizo tata.
“Kuteuliwa
kwa Makonda inatafsiri mpambano utakaokuwepo baina ya Meya mpya na yeye
(Makonda) kwa kuwa, wanaoteuliwa na rais siku zote huwa wanajiona kuwa juu,”
amesema Dk. Lwaitama.
“Hata
Makonda nimemuacha Dar es Salaam ili wabaya wake wamuone akipanda cheo, wenye
chuki wajinyonge zaidi,” amenukuliwa Rais Magufuli wakati akiweka jiwe la
msingi la ujenzi wa kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi namba mbili.
Amesema
Dk. Lwaitama, Rais Magufuli anatakiwa kufanya kazi bila upendeleo kwa kuwa
lengo ni kuwatumikia wananchi na si vinginevyo.
Dk.
Lwaitama anasema hayo wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikilitumbikiza taifa
kwenye sintofahamu ya kisiasa na kwamba, ni wakati wa wananchi kukataa utumwa,
Dk.
Lwaitama anasema, wananachi wanapaswa kuondoka kwenye minyororo ya utumwa na
kusimama katika kuhakikisha wanapigania haki pale inapoonekana kupokwa na
watawala.
Anatoleo
mfano ushindi wa vyama vinavyoundwana ukawa kuchukua Umeya wa Jiji la Dar es Salaam
ambapo ndio Mji Mkuu wa Kibiashara Tanzania na kwamba, hatua hiyo inaanza
kufungua minyororo.
“Wananchi
wanatakiwa kujiandaa kimabadiliko na kuukataa utumwa kwani kwa muda mrefu
walikuwa utumwani kwa kuongozwa na chama kimoja,” anasema Dk. Lwaitama.
Anasema,
wananchi wa Dar es Salaam amekuwa wakijiuliza sababu za kughairishwa uchaguzi
huo mara kwa mara “yote hii ni kwa sababu CCM inang’ang’ania madaraka.”
Akizungumza
na mtandao huu leo Dk. Lwaitama anasema jeuri ya watawala wa nchi hii inatokana
na ubovu wa Katiba na kwamba, udhaifu huo unakwenda mbali ikiwa ni pamoja na
kuteua viongozi wabovu.
Miongoni
mwa viongozi anaowaona kutokuwa na mantiki ya kuwepo kwao licha ya rais kuwa na
mamlaka ya kuwateua ni pamoja na Wakuu wa Mikoa.
“Binafsi
sioni kama kunahaja ya kuwa na wakuu wa mikoa wala wakuu wa wilaya kwani hao
wanaonekana kuwepo kwa ajili ya kujitengenezea ulaji tu.
“Lakini
kazi kubwa inatakiwa ifanywe na Meya wa Jiji ambaye ni mchaguliwa wa wananchi
kwa kupitia madiwani.”
Dk.
Lwaitama anasema, “Inatakiwa tukubali kurudi katika Katiba ya Warioba ili
kuondoa mfumo huu wa kuwa na viongozi wengi ndani ya mkoa mmoja.
“Tunatakiwa
kubaki na Mkurugenzi wa Jiji na Meya wa jiji tu ambaye amebeba ndoto za
wananchi na sio Mkuu wa Mkoa ambaye ameteuliwa tu.”
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline

No comments
Post a Comment