Zinazobamba

NEC YAWAONGEZEA WABUNGE CHADEMA NA CCM,SOMA HAPO



MWENYEKITI WATUME YAUCHAGUZI JAJI MSTAAFU DAMIAN LUBUVA .tum





NA KAROLI VINSENT
TUME ya Taifa Uchaguzi Nchini (NEC) imewaongeza Wabunge  wanawake watu wa viti Maalum kwenye Bunge la Jamhuri wa Muungano,  Wabunge hao ni Lucy OWENYA kutoka chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), na Oliver Senguruka ,Rita KABATI kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM)

Akizungumza na waandishi wa habari Mapema hii leo jijini Dar es Salaam ,Mwenyekiti wa NEC  Jaji mstaafu Damian Lubuva amesema wabunge hao wa viti Maalum wametokana na  Majimbo ya manane ya uchaguzi wa Ubunge ambayo uchaguzi wake ulihairisha Octoba 25 mwaka jana kutoka na tatizo mbali mbali,

‘’Uteuzi huu unafuatia kiako cha tume ya uchaguzi Novembar 11 Mwaka jana ambapo wabunge 113 wanawakew aliteuliwa kuwania viti maalum ,kati yabunge hao walioteuliwa walikuwa 110 viti vitatu vilibakizwa katika majimbo manane yaliyo aihirishwa yakisubiri uchaguzi kwa sababu mbalimbali ‘’Amesema Jaji mstaafu Lubuva .

Jaji Mstaafu  Lubuva amesema kuwa uteuzi huo ulihusisha vyama vitatu ambavyo vilifikisha asilimia 5 CCM 8,3332,953.,Chadema 4,627,923 .Wakati CUF Ilipata kura 1,257,051.


No comments