MAHABA YA JECHA KWA DK SHEIN YATIMIA,HAMAD RASHID AUMBUKA,SOMA HAPO KUJUA
![]() |
| Dk. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar aliyeshinda kwa asilimia 91 |
KILELE cha mahaba ya Jecha Salim Jecha, Mwenyekiti
wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) yametimia
baada ya kumtunuku Dk. Ali Mohammed asilimia 91 ya ushindi, anaandika Happyness Lidwino.
Dk. Shein leo ametangazwa na
ZEC kuwa mshindi wa uchaguzi wa marudio uliofanyika visiwani Zanzibar baada ya
ule wa tarehe 25 Oktoba mwaka jana kufutwa kinyume cha sheria.
Uchaguzi
huo umefanyika jana huku kukiwa na hali ya wasiwasi kutokana na Chama cha Wananchi
(CUF) kuendelea na msimamo wake wa kutoshiriki uchaguzi huo.
Kabla
na baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Zanzibar imepoa, hakuna shamra wala
nderemo isipokuwa kwenye maeneo ambayo vikundi vidogo vilijikusanya na kuanza
kupiga yowe.
Jecha
amemtangaza Dk. Shein (CCM) kuwa ndiye mshindi wa kwanza kwa kura 299,982 sawa
na asilimia 91.
Akitangaza
matokeo hayo, Jecha amemtangaza Hamad Rashid Mohamed (ADC) kushika nafasi ya
pili kwa kura 9,734 sawa na asilimia 3.0.
Awali
Hamadi alidai kwamba, kutokana na Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa mgombea
urais wa CUF kususia uchaguzi, angeweza kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK) endapo angefikisha asilimia 5 kwa
mujibu wa Katiba ya Zanzibar.
Kutokana
na kushindwa kufikisha asilima 5 kwenye uchaguzi huo, Hamad ambaye alifukuzwa
na CUF kutokana na tuhuma za usaliti katika chama hicho, ndoto zake zimefeli.
Jecha
amemtangaza Maalim Seif (CUF) kupata kura 6,076 sawa na asilimia 1.9 ambapo
amedai kwamba, wapiga kura walikuwa 503,580 ambapo jumla ya kura zilikuwa
341,885 sawa na asilimia 7.9 huku kura zilizoharibika ni 13,538 sawa na
asilimia 4.0 na kura halali zilikuwa 328,327 sawa na asilimia 96.0.
Majimbo
mbayo Shein amepata kura nyingi ni pamoja na Chonga kura 3598, Chake chake
4551, Ziwani 2890 na Ole kura 3818.
Matokeo
hayo yametangazwa leo ikiwa baada ya saa 30 tangu kupigwa kwa kura, ambapo leo
matokeo yametangazwa katika Ukumbi wa Salama Hall Bwawani ambapo
watu mbalimbali walihudhulia wakiwemo waangalizi wa ndani ambao pia walionekana
kutokuwa na shamra shamra na matokeo hayo.
Hata
hivyo matokeo hayo pia yametangazwa huku baadhi ya wagombea kutokuwepo ndani ya
ukumbi huo jambo ambalo limeibua maswali mengi kwa wananchi.
Hata
hivyo, utangazwaji wa matokeo hayo umewashangaza wengi kutokana na kutokuwepo
kwa mawakala wa vyama vingine isipokuwa CCM pekee.
Imebainika
kuwepo kwa wanaojiita wasimamizi kwenye uchaguzi huo lakini pale walipoulizwa
chama wanachokiwakilisha, alishindwa kutaka anachokiwakilisha

No comments
Post a Comment