CUF YAMUONYA RAIS MAGUFULI NA DK SHEIN WAKE,YASEMA YATAKAYOTOEKA ZANZIBAR ASILAUMIWE MTU,SOMA HAPO KUJUA

JOTO la kisiasa
visiwani Zanzibar halijapoa na sasa Chama cha Wananchi (CUF) kinakuja na tamko
zito hivi karibuni, anaandika Michael Sarungi.
Chama hicho kinaeleza kuwa, maisha ya dhiki,
wasiwasi, mashaka na unyama uliokithiri katika baadhi ya nchi zinazotawaliwa na
ugaidi duniani yanatokana na watawala kudhani kwamba wao ni sehemu ya familia
ya Mungu.
Magdalena Sakaya, Naibu Katibu Mkuu wa CUF-Bara ameueleza
mtandao huu kuwa, nchi za Nigeria, Somalia na nyingine Afrika zimetawaliwa na
vitendo vya kigaidi kutokana na serikali zao kudhulumu wananchi wao jambo
ambalo limewapa mwanya magaidi kupata wafuasi.
“Hata haya matukio mengi ya kigaidi tunayoyashuhudia katika nchi
kama Nigeria, Somalia na kwingine ni matokeo ya watawala kudharau matakwa ya
wananchi kwa kudhani kuwa, wao ndio wenye maamuzi dhidi ya maisha yao ya kila
siku,”
anasema na
kuongeza, matakwa ya Wazanzibari yamepuuzwa.
Amesema, demokrasia ni utawala wa watu, uliowekwa na watu na kwa
ajili ya watu tofauti na hapo ni udikteta uchwara.
Amesema pamoja na Tanzania kuridhia mikataba mingi ya Umoja wa
mataifa juu ya amani, lakini imekuwa bingwa wa kuikanyaga.
“Demokrasia maana yake ni utawala wa watu, uliowekwa na watu kwa
ajili ya watu, kinyume cha hapo ni udikteta unaolenga kulinda maslahi ya watu
wachache,” amesema Sakaya.
Amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizo na amani kwa
kipindi kirefu na kuwa, tuendako huenda mambo yakawa tofauti.
“Hapa nchini kuna watu wanadhani wana ukoo na Mungu kwa kudhani
kuwa Tanzania haiwezi kutawalika bila yao, huko ni kujidanganya, ipo siku
ukweli utajitenga na uongo,” amesema Sakaya.
Amesema, wanatarajia kukutana kama chama na kutoa msimamo mzito
juu ya ukandamizaji wa haki za wananchi uliofanyika visiwani Zanzibar ikiwa ni
pamoja na baadhi ya wanaCUF kubambikiwa kesi, kuswekwa rumande bila sababu.
“Tunatarajia kukutana kama chama na kutoa maamuzi mazito juu ya
mstakabali wa Zanzibar na Tanzania nzima kwa ujumla,” amesema Sakaya.
Amesema viongozi wengi wa kisiasa kwa sasa wanaotanguliza
maslahi binafsi badala ya wananchi “na ndio maana dunia nzima imeshuhudia sauti
ya wengi ikikataliwa visiwani Zanzibar.”
No comments
Post a Comment