Zinazobamba

WAZIRI MBARAWA ATANGAZA KIAMA WATENDAJI WA TANROAD,ASEMA ATAKUWA MBOGO ZAIDI YA MAGUFULI,SOMA HAPO KUJUA

 

 NA KAROLI VINSENT
WAZIRI wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi,Profesa Makame Mbarawa amewatangazia kiama watendaji wa Wakala wa barabara nchini,(TANROAD) kwa kusema hatasita kumchukulia hatua kali kwa  mtendaji yeyote atakaye kwenda kinyume na kasi ya Rais John Magufuli,
Hata hivyo Waziri Mbarawa amewaonya wakandarasi wa barabara nchini ambao wamezoea kutengeneza barabara zenye chini ya kiwango kwa kuwaapia atakula nao sahani moja.
Akizungumza  leo jijini Dar es Salaam na Viongozi pamoja na wakandarani kutoka ndani ya (TANROAD)  alipofanya ziara ya ofisi hapo,ambapo amesema kwa sasa ndani ya ofisi za wakala wa barabara kumekuwa na watu wasiokuwa waaminifu ambao wanahusika kutengeneza barabara zisokuwa na viwango ambazo zimekuwa zikitumika garama kubwa huku baadae kwa mda mfupi zikiharibika na kuipa serikali hasara kubwa.
“Leo mtandaji anaaminiwa na serikali kwa kusimamia barabara unakuta mtendaji huyo anashirikiana na watendaji wa serikali ili kuhujumu barabara nchini,sasa nataka niwaambie kuwa sahivi nitakuwa mkali,na kama mtu unakaidi basi sitashindwa kukuchukulia hatua kwani utakuwa unarudisha kasi ya Rais wetu”amesema Waziri Mbarawa.
Waziri mbarawa amewataka wakandarani kushirikiana katika ujenzi wa kwanza wa barabara ya juu yaani (Frayover)ambayo ni kwa mara ya kwanza inajengwa nchini hususani mkoa wa Dar es salaam kwa kuwataka kuonyesha ushirikiano wa juu kwa wakandarasi wakigeni ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika salama.
Aidha,Waziri Mbarawa aliwatoa wasiwasi wakandarasi ambao walikuwa wanaidai serikali kwa kusema tatizo hilo ni la mda mfupi kwani serikali ya awamu ya tano itahakikisha inalimaliza tatizohilo.
“Ninachowaomba ondeeni wasi wasi kuhusu madeni haya ya wakandarasi kwani kwa sasa mmeona waote jinsi serikali ya awamu ya tano ilivyovunja katika kukusanya kodi tumeshuhudia tumepata zaidi ya trioni 1.4 kwa mwenzi,kwahiyo tunauwezo wa kuyalipa madeni yote”
Katika hatua nyengine Waziri Mbarawa alifanya ziara katika ujenzi wa upanuzi wa barabara kutoka mwenge jijini dar es salaam hadi Morocco jijini  hapa,huku waziri huyo akifurahishwa na kasi ya ujenzi wa barabara hiyo kwenda kwa kasi kubwa,
Barabara hiyo ambayo imejengwa kutokana na fedha zilizotakiwa zitumike kwenye shuhuri ya kusherekea uhuru ya tehere 9 Desemba ambao Rais Magufuli alifuta sherehe hizo akiwataka Watanzania kujumuika kwenye usafi.

Hakuna maoni