Zinazobamba

WAISLAM CHINI WALAANI MAUAJI YA MTETEZI WA DINI YA KIISLAM NCHINI SAUDI ARABIA,SHEIKH JALALA ATOA YA MOYONI,SOMA HAPO KUJUA

Pichani ni Sheikh Hemed Jalala  ambaye ni Kiongozi wa chuo cha kiislam  cha (Hawaza) Imam Swadig, Sheikh huyo pia  ambaye ni mmoja wa viongozi wakuu wa kiroho wa  wailsamu dhehebu la shia Ithna asherri ya Tanzania akizungumza na wahanabari hawapo pichani akilaani mauaji ya Mwanazuoni wa kiislam kutoka nchini sauda Arabia


WAISLAM  nchini wamelaani vikali kitendo cha serikali ya Saudi Arabia cha kumuua mwanadhuoni  Ayotollah Sheikh Bagir Nimr ambaye alikuwa anawatetea wanyonge na waislam nchini humu.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
       Akisoma  tamko la kulaani kitendo hicho, Sheikh Hemed Jalala  ambaye ni Kiongozi wa chuo cha kiislam  cha (Hawaza) Imam Swadig, Sheikh huyo pia  ambaye ni mmoja wa viongozi wakuu wa kiroho wa wailsamu dhehebu la shia Ithna asherriya Tanzania
     Ambapo amesema waislam nchini wamepokea kwa masikitiko makubwa kwa  kitendo cha kinyama cha watu kumuua kwa kumchinja  hadharani mtetezi huyo baada ya kuhukumiwa kifo na serikali ya nchi hiyo.
     Amesema adhabu ya kifo aliyopewa mwanadhuoni huyo ni ya kionevu kwani haendani na mafunzo ya dini ya kiislam.
      “Yaani huyo Sheikh Nimr amehukumiwa baada ya kutetea haki ya waislam ikiwemo kupata  haki ya kusari mara tano kwa siku ambayo nchini Saudi Arabi hawapati nafasi hiyo,amekuwa anatetea haki ambayo serikali yake ilikuwa haiwatendei haki wananchi wake,lakini leo serikali hii ikaona njia sahihi ya kumyamazisha ni kumhukumu kifo “amesema Sheikh Jalala.
Waislam wa msikitiwa Kigogo Post Jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye sara ya kulaani unyama huo

     Sheikh Jalala akiongea kwa uchungu amesema inasikitisha kuona nchi kama Tanzania ambayo inamuunganiko wa dini mbali mbali lakini bado waislam wanapata haki ya kuaabudu mara tano kwa siku lakini nchi ya Saudi Arabia ambayo ni ardhi yake imetaliwa na dini hiyo lakini waislam hawapati nafasi ya kuabudu mara tano kwa siku jambo analosema linakwaza mtume Muhamed ambaye alitaka kila mtu apewa haki ya kuabudu.
     “Makosa yalitajwa na serikali ya Riyadhi juu ya Ayatollah Nimr na wenzake kwamwe hayakustahili adhabu hiyo,kumuua kiongozi mwenye wafuasi kwa kosa la kudai haki za wanyonge  ni kuchochea vurugu”amesema Sheikh Jalala.
    Sheikh Jalala amebainisha kuwa binadamu ni kiumbe aliyehuru kutokuwa na  minyororo ya ukandamizaji na utumwa katika Nyanja zote,yuko huru kutokuwa  na utumwa wa kifikra, huku akihoji ni kuwa ni kivipi karne hii ambayo uelewa juu ya masuala ya binadamu na maswala ya kielimu yameshika kasi kwanini yatokea mambo kama haya.
      Vilevile Sheikh Jalala ameitaka Dunia kuingilia kati vitendo vya kinyama vinavyofanywa na serikali ya Saudi Arabia kwa kunyima uhuru wa haki za kuishi pamoja na kutoa maoni.


   Mwanazuoni Ayatollah Sheikh Bagir Nimr aliuwa tarehe 2/1/2016 baada ya kutolewa hukumu na serikali ya  Saudi Arabia baada ya kuhukumu kwa kosa la kushiriki kudai hakiiii ya uhuru wa wananchi kuchagua viongozi wao kwa kura badala ya kuongozwa kifalme,
Kosa jengine ni  kudai haki za binadamu ziheshimiwe kwa kuwa kuna matabaka  ndani ya nchi ynanyima haki zao za msingi,pamoja na kutolewa na kuachiwa huru wafungwa wakisaisa waliokamatwa kwa kudai mabadailiko ya kiungozi katika serikali na haki ya kuchagua viongozi wao.
 

Hakuna maoni