VIJANA WA JKT WAMUANGUKIA RAIS MAGUFULI,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
UMOJA wa Vijana waliopata mafunzo kupitia Jeshi la
Kujenga Taifa (JKT), wamemuomba rais Dk.John Magufuli kusikiliza kilio chao cha
ajira, kutokana na ugumu wa maisha unaowakabili.
Hatua hiyo inatokana na jitihada za vijana hao zaidi
ya 300 kugonga mwamba katika utawala wa rais mstaafu Jakaya Kikwete baada ya
kufanya maandamano mwaka jana kwa shinikizo la kukutana naye ili kumweleza
tatizo hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar
es Salaam, Katibu Msaidizi wa Umoja huo, Mathias John alisema kupitia kauli
mbiu ya rais Magufuli ya ‘Hapa Kazi Tu’ wanamuomba awatumie katika ujenzi wa
taifa.
Alisema kauli mbiu hiyo inadhihirisha ni jinsi gani
taifa na wananchi wake wanaweza kuendelea kwa kuchapa kazi, hivyo azitumie
nguvu kazi zao katika sekta mbalimbali za kuinua uchumi.
“Kutokana na mafunzo tuliyopata katika kipindi cha
takribani miaka mitatu, tunaamini nguvu kazi yetu ikitumiwa vilivyo basi
tutapiga hatua kubwa, lakini zikiachwa ndio uzaa athari ikiwemo matukio ya
kiuhalifu,”alisema.
Akitolea mfano wa athari, John alisema waliwai
kutishia kufanya maandanamo ya siku tatu mfululizo kudai wapatiwe ajira,
kutokana na kutojua hatma ya maisha yao jambo lililozaa chuki baina yao na
utawala wa kipindi hicho.
Naye mmoja wa wajumbe wa Umoja huo, Omary Said
alieleza kuwa vijana waliohitimu mafunzo hayo kwa sasa wanakabiliwa na hali
ngumu ya kimaisha, huku baadhi yao wakiwa wapo mahakamani.
“Endapo nguvu kazi zetu zingetumika vyema ikiwemo ya
wahitimu wenzetu sita waliopo mahabusu akiwemo Mwenyekiti wetu George Mgoba
ambaye yupo katika hali mbaya, basi tungepandisha uchumi wetu kwa kasi kubwa;
Pi “Vijana wengi wamekuwa wakipelekwa
JKT na kuahidiwa kupatiwa ajira, lakini toka mwaka 2000 hadi 2014 wameajiriwa
vijana wachache na wengine tumekuwa tukiachwa,”alisema.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni