TUKIO KUBWA LEO ALILOFANYA KAMANDA SIIRO DAR LEO,BOFYA HAPO KUJUA ZAIDI
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Simon Sirro,
akizungumza na wadau mbalimbali juu ya kufanisha uzinduzi wa Stika
maalumu yenye ujumbe wa kutokomeza mauaji ya watu wenye Albinism,leo
jijini Dar es Salaam.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Simon Sirro,
akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Stika maalumu yenye ujumbe wa
kutokomeza mauaji ya watu wenye Albinism jijini Dar es Salaam,kulia ni
Mwenyekiti wa Albno Enteprises of Dar es Salaam Michael Lugendo.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Simon Sirro,
akupokea tuzo kutoka kwa Mwenyekiti wa Albino kutoka Enteprises of Dar
es Salaam, Michael Lugendo leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Simon Sirro,
akionesha Stika mara baada ya uzinduzi wa wa Stika maalum yenye ujumbe
wa kutokomeza mauaji ya watu wenye Albinism,leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu
ya maofisa mbalimbali wa Jeshi la Polisi waliofika katika uzinduzi wa
Stika maalum yenye ujumbe wa kutokomeza mauaji ya watu wenye
Albinism,leo jijini Dar es Salaam.
Waandishi
wa habari wakimsikiliza Kamanda wa Polisi Kanda Maalimu ya Dar es
Salaam, Naibu Kamishna, Simon Sirro, leo jijini Dar es Salaam.
TAASISI ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino)
‘Enterprises of Dar es Salaam-AED’ kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam, leo jijini Dar es Salaam imezindua stika maalumu
yenye ujumbe wa kutokomeza mauaji ya watu hao.
Stika hiyo imebeba ujumbe wa
“Ewe ndugu Mtanzania tuungane na Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli, Jeshi la
Polisi na wadau mbalimbali katika kutokomeza mauaji ya ndugu zetu wenye
albinism. Kwa pamoja tunaweza.”
Uzinduzi
wa stika hiyo unalenga kuhamasisha jamii kuwapenda, kuwafariji na
kuwahakikishia usalama wao albino pia kuwa huru kifikra kwa kujilinganisha na
watu wasio na ulemavu wa ngozi.
Akisoma
risala iliyoandaliwa na taasisi ya AED mtunza fedha wa taasisi hiyo Mwamvua
Kambi kwa mgeni rasmi Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Simon
Siro amesema kuwa, kutokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi ni kazi
ngumu inayohitaji ushirikishwaji wa kila mtu.
Mwamvua
amesema kuwa watu wenye ulemavu wa ngozi nchini wanakabiliwa na mauaji ya aina
tatu ambayo ni mauaji ya kisaikolojia yanayomgusa kila albino hasa kwa
kushuhudia vitendo vya kikatili vya ukataji viungo vya wenye ualibino
vilipoibuka.
Pia,
mauaji yanayosababishwa na saratani ya ngozi ambayo hutokana na ukosefu wa
mafuta ya ngozi yanayo kinga athari za mionzi ya jua na vikingia jua. Vilevile
mauaji ya kukatwa viungo ambayo jamii inayatambua hadi sasa.
Mkurugenzi
wa taasisi hiyo Michael Lugendo amesema mikakati itakayotumiwa kufikia lengo la
kutokomeza mauaji hayo ni pamoja na kusambaza stika kwa njia ya nyumba za
ibada, kutumia mawakala nchi nzima, kutumia vituo vya kudumu katika maeneo
yenye watu wengi.
Pamoja
na kutumia ligi ndogo za mpira wa miguu kama ligi iliyoanzishwa inayoitwa
Balozi Samata Cup ambayo lengo lake ni kuibua vipaji, kutoa elimu kuhusu
masuala ya albinism na kusambaza stika. Ligi hiyo itaanza tarehe 30 Januri
mwaka huu.
“Tuna
mpango wa kuteua mabalozi wengine kutoka makundi mbalimbali ili kushirikiana na
Mbwana Samata kuleta matokeo chanya katika kubadilisha historia ya wenye
ulemavu wa ngozi Tanzania,” amesema Lugendo.
Akizindua
stika Kamanda Simon Siro amesema kuwa, ni wajibu wa kila mtu kwa nafasi yake
kuhakikisha albino wanaishi kwa amani na usalama pia aliwahakikishia kuwa jeshi
la polisi litatoa ushirikiano katika kudhibiti mauaji hayo.
“Kuna
baadhi ya maeneo bado ya dhana potofu ya kuamini kuwa kupata kiungo cha albino
ni kuwa tajiri, huu si ukweli sababu tatizo la ualbino ni la kibaiolojia. Mikoa
ya kanda ya ziwa inaongoza kwa kuwa na kesi nyingi za mauaji ya kikatili ya
albino. Inabidi mikoa hiyo ipewe elimu ya kutosha,” amesema Siro na kuongeza:
“Vyombo
vya dola vinawajibika kupata taarifa za matukio hayo na kuwafanyia kazi
watuhumiwa kwa kuwachukulia hatua kali za kisheria ili kutokomeza tatizo hili.”
Siro
amewataka wananchi na wenyeviti wa serikali za mitaa kujua idadi ya albino
waishio kwenye maeneo yao, kuwahakikishia ulinzi pamoja na kutoa taarifa
wanapopata matatizo na kutoa taarifa mapema kama kuna watu wenye nia mbaya nao
ili kuzuia matukio hayo.
Viongozi
wa dini wametakiwa kutoa elimu ya kiroho kwa waumini wao juu ya athari za
mauaji ya kikatili ya albino na kutoa msaada kwa albino waliokumbwa na janga
hili la ukatwaji wa viungo vyao.
Taasisi
imewaomba wadau mbalimbali kama wasanii, wanasiasa, viongozi wa taasisi za
kidini na wafanyabiashara kutoa msaada watakaopo hitaji msaada wao wa hali na
mali.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni