Zinazobamba

DKT EDWARD HOSSEAH ATOWEKA NCHINI,AKIMBIA RUNGU LA MAGUFULI,SOMA HAPO KUJUA

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Edward Hoseah

MKURUGENZI  wa zamani wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Dkt Edward Hosseah ameondoka nchini na kuibua sintofahamu.(mtandao huu umedokezwa) Anaandika KAROLI  VINSENT endelea nayo.
     Taarifa za kuaminika ambazo mtandao huu umezipata zinasema Hosseah ameondoka nchini kwa kile kinachoiitwa ni hofu,kutokana na utawala wa Rais John Magufuli ambao unatajwa kujiandaa kumburuza makahamani kutokana na tuhumu lukuki zinazomwandama.
       Dk Hoseah (57) alifukuzwa kazi na Rais Magufuli tarehe 16 desemba ,mwaka huu kwa madai ya kutoridhishwa na utendaji wa kazi yake,
      Katibu mkuu kiongozi ,Ombeni Sefue  alitangaza kufukuzwa kazi  kwa Dk Hoseah kwa kile anachodai kushindwa kuzuia rushwa, na baadaye kubainisha kuwa nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Naibu mkurugenzi wa Takukuru ,Valentino  Mlowola.
         “Ninachokwambia huyu bwana(Hoseah) hayupo nchini kabisa  ameondoka na yupo kwenye nchi moja ya ulaya huko,amefanya hivi ili kuepuka kadhia, maana huyu naye anajua  anaweza kuwa ni jipu linalosubili kutumbuliwa na  utawala wa Magufuli”kimesema Chanzo chetu.
       Kuibuka kwa taarifa hizi,za Dk Hoseah kuondoka nchini zinakuja ikiwa kuna taarifa ya mkurugenzi huyo kutarajiwa kupandishwa mahakamani mda wowote toka sasa kutokana na  tuhuma lukuki ambazo zinamkabili ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka  na kushindwa kuzibiti rushwa nchini,
      Rushwa ambazo  anatuhumiwa Hosseh  ni Kushindwa kuzibiti ni ununuzi wa Rada ,Kashfa ya Richmond  ambapo kamati teule ya Bunge  iligundua kuwepo kwa ufisadi.
        Kashfa nyengine ni ile  iliyoibuliwa na Taasisi ya uchunguzi wa makosa makubwa  ya rushwa (SFO).ilibainiwa kwa baadhi ya vigogo wa Tanzania walipokea rushwa.
       Sanjari hizo pia Hosseah, ameshindwa kuzuia rushwa  katika sakata la Tegeta Esrcow,pia katika kipindi cha miaka 10 alichokaa madarakani Hosseah anatuhumiwa kufumbia macho uporaji wa mabilioni ya Akaont ya madeni ya nje EPA iliyokuwa  Benki kuu (B.O.T)
Pia Kashfa nyengine anayotuhumiwa pia kunyamazi sakata la Ufisadi wa hati fungani ya Benki Stanbik ambapo kumetokea ufisadi wa zaidi trioni 1.2 za kitanzania

Hakuna maoni