Zinazobamba

CHAMA CHA CUF CHAMBANA RAIS MAGUFULI NA SERIKALI YAKE,NI KUHUSU ZOEZI LA BOMOA BOMOA,SOMA HAPO KUJUA


Naibu katibu mkuu wa chama cha CUF  bara Bi. Magdalena Sakaya  akiongea na Waandishi wa Habri(hawapo Pichani) kuhusiana na uchaguzi serikali za mitaa.
Pichani ni Magdalena Sakaya akizungumza na wanahabari hawapo pichani

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimeitaka  serikali ya Rais John Magufuli kuacha kutumia ubabe kwa kuendelea zoezi la bomoa bomoa kwa Wananchi, kwa madai zoezi hilo linakasoro lukiki ambazo zinakwenda na kinyume na haki za binadamu.Aaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
    Kauli ya CUF inakuja ikiwa ni siku moja kupita baada ya ofisi ya Makamu wa Rais kuibuka kutangaza kuhamishia zoezi la BomoaBomoa katika Bonde la mto Msimbazi Jijini Dar es salaam.
    Akizungumza na waandishi wa habari leo mapema jijini Dar es Salaam,Naibu Katibu mkuu wa CUF bara,Magdalena Sakaya amesema Chama chake kimefanya utafiti tangu zoezi la bomoa bomoa lilipoanza na wamebaini zoezi hilo limejaa mapungufu makubwa ambayo anadai yanamtesa mwananchi.
    “CUF tumefanya uchunguzi na kubaini kwamba kuna kundi kubwa la wananchi wamebomelewa makazi yao na kuharibiwa sehemu zao za biashara kimakosa”amesema Bi Sakaya.
   Mheshimiwa Sakaya ameyataja makosa hayo ni maeneo ya makazi ya wanaoishi maeneo ya mto msimbazi akidai kunawakazi wameishi miaka mingi  na wanahati za nyumba, ambapo ameeleza mwaka 2012 walitakiwa kupewa viwanja maeneo ya mwabepande lakini hawakupewa viwanja hivyo anashangaa kwanini serikali inawavunjia,
    Vilevile Sakaya ameendelea kuitupia lawama serikali akidai ndio iliyopelekea wananchi kujenga katika maoneo ambayo anakili ni hatarishi akidai kuwa serikali ilishindwa kusimamia katiba ya nchi.
     “Nchi yetu inakatiba na sheria na inawasimamazi na wafuatiliaji wa utekelezaji wa hizo sheria  ili kuhakikisha wananchi hawastahili kujenga maeneo hayo inakuwaje kipindi chote hicho wananchi  wajenge nyumba zao wameishi kwa miaka takribani 2o eti leo unaibuka na kusema wamekiuka sheria,huu ni uzembe wa serikali”
   Hata hivo,Sakaya ameonesha masikitiko yake kwa Waziri Muungano na Mazingira,Januari Makamba kwa taarifa yake aliyoitoa jana kwa kusema sehemu ya nyumba zilizobomolewa ni zile ambazo watu wake wamekwisha amua kubomoa wenyewe.
     Akipinga hoja hiyo,Sakaya amesema Chama cha CUF kimefanya utafiti kimegundua licha ya nyumba hizo kubomolewa lakini bado wananchi wanaendelea kushia sehemu hiyo iliyobomolewa huku akishangaa kwa kusema kama walikuwa wanabomoa wenyewe mbona wapo wanaishi kwenye nyumba walizobomoa.
“Katiba ya nchi sehemu ya tatu kifungu cha 12 na 13 3 suala la haki na utu wa kibinadamu ni serikali haijazingatia hata kidogo  zoezi la bomoa bomoa kunavitendo dhahiri vya kudhalilisha utu na thamani ya utanzania kwa mfano serikali inabomolea nyumba bila hata kujiridhisha kuwa usalama wa maisha ya watu yanaziingatiwa”ameendelea kuongeza sakaya.
Pamoja na hayo yote,Sakaya ameitaka serikali ihakiki inawapatia huduma za kibinadamu  wakazi wote waliobomolewa nyumba zao na hivi sasa ambao amedai hawana makazi ya kuishi

Hakuna maoni