ALIYESEMA ZANZIBAR AICHUKULIWI KWA KARATASI,AFARIKI DUNIA,NI ASHA BAKARI MAKAME,SOMA HAPO KUJUA
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Zanzibar, Asha Bakari Makame |
MAKAMU Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha
Mapinduzi (UWT) Zanzibar, Asha Bakari Makame amefariki dunia leo huko Dubai. Anaandika Yusuph Katimba … (endelea).
Bi.
Asha alifariki dunia ikiwa ni siku chache baada ya kutoka nchini India kupata
matibabu ambapo taarifa za ndani zinaeleza kwamba, alikwenda Dubai kwa mwanae
kabla ya kurejea visiwani Zanzibar.
Taarifa ya Naibu Katibu Mkuu wa
UWT visiwani Zanzibar, Salama Aboud Talib imethibitisha kutokea kwa msiba huo.
Bi. Asha kabla ya kuwa mwenyekiti
wa UWT visiwani humo, aliwahi kuwa Waziri wa Wanawake na Watoto katika Serikali
ya Awamu ya Tano visiwani Zanzibar chini ya Rais Salmin Amour.
Mwanasiasa huyo pia aliwahi kuwa
mwakilishi katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar kupitia CCM pia aliwama Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba
Hakuna maoni
Chapisha Maoni