Zinazobamba

YANGA YAANZA KUSHIKANA UCHAWI NA WACHEZAJI,YAMTIMUA HARUNA NIYONZIMA,SOMA HAPO KUJUA

Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima (kulia) akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Abdallah Bin Kleb
Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima (kulia) akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Abdallah Bin Kleb


YANGA SC imevunja Mkataba na kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Niyonzima kutokana na mchezaji huyo wa Amavubi kukiuka vipengele vya mkataba wake na klabu hiyo. Anaandika Erasto Masalu … (endelea).
Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha amewaambia Waandishi wa Habari katika Mkutano uliofanyika makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam kwamba Niyonzima pia atatakiwa kuilipa klabu. 
Niyonzima amekuwa katika mgogoro na klabu ya Yanga kwa muda mrefu toka alipochelewa kujiunga na klabu yake, akitokea kwao kuitumikia timu ta Taifa ya Rwanda katika michuano ya kimataifa mapema mwezi huu.
Yanga imefikia uamuzi huyo baada ya kumsimamisha nyota huyo kipenzi cha Wanajangwani, lakini pia ilimhoji kupitia Kamati yake ya Nidhamu na kumpa nafasi kiungo huyo kujieleza.

Maoni 1

Bila jina alisema ...

Tafadhalini Simba msimwache mchezaji huyo almasi