WAZIRI KITWANGA AWASHUKIA WATENDAJI WA UHAMIAJI NCHINI,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi,Charles Kitwanga akizungumza na waandishi wa Habari hawapo pichani leo mara baada ya kumaliza kikao na watendaji wa Idara ya Uhamiaji nchini |
WAZIRI wa Mambo ya ndani ya Nchi,Charlse Kitwanga
ameitaka Idara ya Uhamiaji kutompa mgeni yeyote kibali cha kuishi nchini bila
mgeni huyo kutokuwa na kibali cha kufanya kazi nchini.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Akizungumza
na waaandishi leo Jijini Dar es Salaam, mara baada ya kumalizika kikao na
makamishna watendaji wa Idara ya Uhamiaji nchini,Waziri Kitwanga amesema kwa
sasa kumekuwa na msuguano kati ya Idaya ya uhamiaji ambao ndio wanatoa kibali
cha kuishi nchini na wizara ya Kazi ambao wanatao kibali cha kufanya kazi kwa
wageni nchini.
“Nimewataka idara ya uhamiaji nchini kutompa mgeni
yeyote kibali cha kuishi nchini,mpaka wizara ya kazi watakapompa kibali cha
kufanya kazi nchini mgeni ,kwasababu kumekuwa na wageni ambao wamejaa nchini
ambao hawana shughuli za kufanya jambo linaloweza kuleta uharifu”Amesema Waziri
Kitwanga.
Waziri
Kitwanga ameongeza kuwa katika kukabiliana na tatizo la rushwa kwa watendaji wa
uhamiaji amesema kwa sasa wizara yake pamoja na idara hiyo wako mbioni
kuanzisha mfumo mpya wa utoaji pasi za kuishi, bila ya mwananchi kutoonana na
mtumishi wa uhamiaji,
Ameeleza kuwa
mfumo huo ambao utamfanya mwananchi kujiorodhesha na kufuata hatua zote ikiwemo
kwenda kulipa benki kwa kutumia kupyuta jambo analodai litachangia kuaondoa
Rushwa kabisa,
Aidha,Waziri
Kitwanga ameunda timu ya watu wa uhasibu kutoka wizarani kwake kwenda kufanya
uchunguzi wa matumizi ya fedha katika idaya ya uhamiaji lengo ni likiwa kuzima
mianya ya pesa inayopetea katika idara hiyo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni