Zinazobamba

MAUZO KATIKA SOKO LA HISA DSE YASHUKA TENA,SOMA HAPO KUJUA


NA KAROLI VINSENT
IDADI ya Mauzo katika soko la hisa mkoa wa Dar es Salaam (DSE) kwa wiki hii yameshuka kwa asilimia 67  pamoja na idadi ya hisa kwenye mauzo pia yameshuka kwa asilimia 84 toka milioni 11.6  hadi milioni 1.8 kwa wiki hii.
Hata  hivyo  idadi ya mtaji pia ndani ya soko la hisa pia imeshuka toka trioni 21 kwa wiki iliyopia hadi trioni 20.2.
      Hayo yameelezwa Jana jijini dare s Salaam,na Meneja masoko wa DSE,Patrick Mususa wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo alisema mauzo hayo kushuka kwake kwa wiki hii imechangiwa na hali ya kwenye kaunta ya TBL jambo lilochangia mauzo hayo kushuka,
    Mususa alizitaja kampuni tatu zilizoongoza kwa mauzo  kwenye  kwa wiki hii ni Kampuni ya TBL 39%, benki ya CRDB 26%,TCCL 24% huku kampuni moja iliyojitokeza kwa wiki kwenye soko hilo inayongoza kwa bei ambayo ni Tanzania Media group kwa salimia 7,
     Mususa alisema kuhusu viashiria vya sekta alisema sekta ya viwanda imeshuka kwa asilimia 9,viashiri katia benki ya huduma za benki nayo pia ilishuka kwa asilia 90 jambo analodai limechangiwa na mabadiliko katika Benki ya Exim.
    Hata hivyo Mususa alizungumzia kuhusu uuzaji wa hati fungani iliyowekwa na Benki ya Exim kwa kusema muda wake ni teyari umeshafikia tamati huku akiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika ununuzi wa Hisa katika soko hilo kwa kutumia namba ya simu kwa kubonyeza  *150*30# na kufuata maelezekezo.

Hakuna maoni