VYUO VIKUU NCHINI HATARINI KUFUNGWA,PROFESA MKUMBO AMUANGUKIA MAGUFULI,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Prifesa Kitila Mkumbo |
VYUO vikuu nchini vimetajwa kuwa viko hatarini kufungwa kutokana na kukosa Wanafunzi.Anaadika KAROLI VINSENT
endelea nayo.
Tahadhari
hiyo imetolewa na Mhadhili kutoka chuo kikuu cha Mlimani,Profesa Kitila Mkumbo
wakati wa kuwasilisha mada kwenye uzinduzi ya ripoti iliandaliwa na Taasisi ya
Haki ya Elimu kuhusu maendeleo ya elimu yalitokelezwa na awamu iliyomalizika ua Rais Jakaya Kikwete
ndani ya miaka kumi,
Profesa
Mkumbo amesema kutoka na idadi ndogo ya wanafunzi wanaomaliza kidato cha sita huku vyuo vikuu kuwa vingi basi kutaleta
hatari kubwa ya vyuo vikuu kufungwa,
Amebainisha
kuwa asilimia 25 tu ya wanafunzi ndio wanakwenda
kwenye vyuo vikuu huku idadi kwenda chuo kikuu,huku wengine wakikosa sifa ya
kuchaguliwa kwenda kwenye vyuo hivyo,pamoja na Ada za masomo jambo analodai
kuwa limechangia vyuo vingi vikuu kukosa wanafunzi.
Hata
hivyo,Profesa Mkumbo ameishauri Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli kuliangalia suala hilo kwa
umakini ili kuweza kuliokoa Taifa kwenye sekta ya elimu hususani suala la
Udahili wa wanafunzi.
Naye
Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ambaye
alikuwa Waziri kivuli wa Wizara ya Elimu kwenye utawala wa awamu ya nne,Suzan
Lyimo amsema hali ya elimu kwa sasa nchini
ipo katika hali mbaya baada ya serikali kushindwa kusimamia elimu kwa dhati,
Amesongeza
kusema kuwa kutokuwa na vyuo bora vya ufundi nchini ni tatizo,huku akimtupia
lawama Rais mstaafu Jakaya Kikwete kushindwa kutekeleza ahadi yake ya kujenga
vyuo vya ufundi kila kata.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Haki Elimu John
Kalage amesema ili elimu iokolewe hapa ilipo ni kwa serikali kuangalia
kwa umakini Bajeti ya Elimu nchini kwa kuondoa matumizi makubwa yasiyo na
lazima badala yake pesa hizo zielekezwe kwenye masuala ya maendeleo ya elimu.
Maoni 1
Dahh hivi ni lazima kila mtu awe anaandika mbona kilichoandikwa hakieleweki?
Chapisha Maoni