TUNDU LISSU AWAGALAGAZA WAPINZANI WAKE,SOMA HAPO KUJUA
JAJI wa mahakama
kuu ya Dodoma jaji Seheni, ametupilia mbali maombi ya Jonathan Njau (CCM)
ya kutaka apunguziwe gharama ya uendeshaji wa keshi ya kupinga uchaguzi nafasi
ya ubunge dhidi ya mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu (Chadema). Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).
Katika kesi hiyo namba 1 ya mwaka 2015 Njau
aliomba asitoe kiasi cha shilingi milioni 15 ambacho kipo kisheria kutokana na
kutokuwa na hela kwa madai kuwa hela hizo ni nyingi na hawezi kuzipata kutokana
na ukata alionao baada ya uchaguzi.
Akisikiliza kesi hiyo jaji Sheheni alisema haiwezekani kupunguza
gharama hiyo kwani hipo kisheria.
Awali Lisssu aliweka pingamizi kwa madai kuwa maombi pamoja na
viapo vyote vimekosewa na kuna kila sababu ya kupeleka fedha hizo ili kukithi
matakwa ya kisheria.
Akizungumza nje ya Mahakama Lissu amesema: “Watu walileta maombi
ya kusamehewa kulipa fedha za gharama za kesi sh milioni 15 yule bwana
anayetishia wapiga kura wangu kuwa yeye ni bilionea alileta maombi ili
asamehewe kwa madao ameishiwa ,sasa ameleta maombi na viapo vimekosewa na
hajatimiza masharti ya kisheria.
“Kwa hiyo nilimwekea pingamizi kuwa maombi na viapo vilivyo
letwa mahakamani havijafuata sheria na tukaomba yafutiliwe mbali na jaji
ametukubalia kwa hiyo hakuna maombi hapa” amesema Lissu.
Amesema kutokana na kufutiliwa mbali maombi hayo sheria inaeleza
kwamba isipopelekwa sh.milioni 15 kesi hakuna.
Lissu amesema kutokana na hali hiyo hakuna kesi ya msingi hakuna
hadi hapo itakapokuwa imepelekwa fedha hiyo.
Lissu anasema kuwa Njau kamtuhumu kuwa aliwaonga viongozi wa
dini, alinywesha watu pombe,alihonga mashuleni na kuwapiga wapiga kura.
Amesema tuhuma ambazo Lissu ametuhumiwa zinalenga kumzuia
kufanya siasa kwa kipindi cha miaka 10. Hata hivyo alisema wakili Wasonga
ambaye anamtetea mteja wake ambaye aligombea ubunge kupitia CCM alisha wahi
kufanya makosa yale yale katika kesi ya mwaka 2010.
“Mwaka 2010 Wasonga alileta makosa yale yale yenye makosa yale
yale kama haya ambayo yameletwa leo yenye makosa ambayo yamefutwa,” amesema.
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni