HABARI KUBWA LEO-MAKONTENA 11,884 NA MAGARI 2,019 VYAPOTEA BANDARINI TENA,KAMPUNI YA AZAM NA WENZAKE WAZIDI ITAFUNA NCHI,WAZIRI MBARAWA AISHIWA PUMZI,SOMA HAPO KUJUA
WAZIRI wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Profesa
Makame mbarawa ameibua ufisadi wa kutisha ndani ya Mamlaka ya Bandari nchini TPA,baada ya kubaini upotevu wa makotena 11,884 pamoja na magari
2,019 kwenye Bandari kavu 7.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Waziri
Mbarawa ameyaibua hayo leo alipofanya ziara ya kushtukiza ndani ya (TPA) ambapo amesema mara baada ya Waziri mkuu,Kassim Majaliwa
kufanya ziara Bandarini hapo mwezi mmoja uliopita alibaini upotevu wa Makotena
2431yalikuwa kwenye Bandari kavu,
Amedai
kuwa Baada ya Majaliwa kubaini upotevu akaiamulu TPA kufanya ukaguzi wa
kina,ambapo leo uchunguzi huo umebaini kuna upotevu wa
Makontena mengine 11,884 yenye thamani ya bilioni 48
na magari 2019 yenye thamani ya bilioni 1 yakiwa yamepita bila kulipwa tozo (wharfage).
Waziri Mbarawa amezitaja Bandari kavu hizo zilizohusika na Kashfa
hiyo ni ya Azam yamepotea 295 , PMM makontena 779,Kampuni ya JEFAG makontena
1450,TRH makontena 4,424,AMI makontena 4,384,
Makampuni mengine
ni MOFED makontena 61 pamoja na Kampuni ya DICD 491,
Sanjari na
Upotevu huo wa Makontena pia Waziri Mbarawa ameyataja makampuni mengine
yalihohusika na upotevu wa Magari 2,019
ni TALL 309,CHICAS magari 65,HESU 1,359,SILVER magari 97.
HATUA
ZILIZOCHUKULIWA.
Waziri
Mbarawa amesema baada ya kubaini upotevu hadi kufikia leo Desemba 29 mwaka huu
watumishi 7 kati ya 15 waliokuwa wamehusika na ukusanyaji wa mapato ya Wharfage
katika ICD na CFS wamekamatwa na kufikishwa polisi ili waweze kuchukuliwa hatua
za kisheria huku wengine nane wakitafutwa.
Sanajari na
hatua kwa watumishi hao pia,Waziri Mbarawa amewapa siku 7 makapuni ya uwakala
243 yaliohusika na upotevu huo wawe wamelipa kodi hizo,
Vilevile Waziri Mbarawa amesema Serikali ya awamu ya
tano haita mvumilia mfanyakazi yeyote wa Mamlaka ya usimamizi wa Bandari
Tanzania awe mkebwa au mdogo ambaye ataendelea kujihusisha na upotevu wa mapato
basi atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni