ZANZIBAR APATOSHI SASA,WAJUMBE WAWAKILISHI WALIPUKA NAO NA KUMVAA JECHA,SOMA HAPO KUJUA
![]() Baadhi ya wawakilishi waliochaguliwa kuwakilisha baraza la wawakilishi Zanzibar waliohudhilia katika mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. ![]() |
Naibu katibu mkuu wa Chama Cha wananchi CUF, Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na waandishi wa habari leo katika mkutano wa waandishi wa habari leo kuhusiana na wabunge wa baraza la wawakilishi Zanzibar kumwomba rais wa jamhuri ya muungano kuwaapisha ili waanze kufanya kazi yao kwaajili ya kuwawakilisha wananchi wa majimbo yao |
WAJUMBE wa
Baraza la wawakilishi wa Zanziba kupitia Chama cha Wananchi (CUF), wameitaka
tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), kutengua tamko la mwenyekiti wa tume hiyo. Anaandika Faki Sosi… (endelea).
Hayo
yamesemwa na Mwakilishi mteule wa Jimbo wa Mgogoni Abubakar kwa niaba ya
wawikilishi hao 26
Amesema kuwa
mwenyekiti huyo amekwenda kinyume na katiba na sheria ya nchi hiyo kwa
kufutamatokeo hayo.
Khamis amesema kuwa uchaguzi ulifanyika vizuri na kuwapa nafasi
wananchi wa Zanzibar waliojiandikisha katika daftari la kudumu kuchagua
kiongozi wanayemtaka na baadaye upigaji kura ulipomalizika kazi ya kuhesabu
ilikwenda vizuri matokeao yalitangazwa kwa kila jimbo pia hakukuwa na
malalamiko ya chama chochote cha kisiasa kilichoshiriki kwenye uchaguzi huo.
Aidha aliongeza
kuwa kuwasheria ya Uchaguzi Zanzibar namba 11 ya mwaka 1984 imetoa uwezo na
mamlaka ya kusimamia na kuendesha uchaguzi wawakilishi na masheha(Madiwani)kwa
msimamizi wa jimbo .
“Hakuna sehemu
yoyote katika katiba ya Zanzibar ya 1984 inayotoa mamlaka kwa mwenyekiti tume
ya uchaguzi au msimamizi wa uchaguzi kufuta matokeo halali ya uchaguzi” amesema
Abubakar Khamis Bakari.
Amesema kuwa
imewashangaza sana kuona uchaguzi huo umeenda sambamba na ule wa wabunge wa
Jamhuri wa muungano wa Tanzania na kutumia daftari moja la kujiandiandikishia
wapikura ikiwa uchaguzi mmoja unadosari mwengine hauna dosari inaitashaka.
Wawakilishi
walioandamana naye ni pamoja na wa majimbo ya Mto Pepo, Malindi, Chukwani, Mgogoni,
Ole, Kijini, Wingwi, ChakeChake, Micheweni, Gando, Chambani, Mtambile, Tumbe,
Mwembe Kwelekwe, Mpendae, Wete, Chonga, Kiwani Ziwani, Kojani, Bumbwini,
Mkoani, Wawi, Mtambwe, Nungwi na Konde.
Kuibuka
kwa wakilishi hao kunakuja ikiwa ni teyari nchi wahisani wakiongozwa na
Marekani wakiwa wameitishia serikali ya Rais John Magifuli kuwa wataskitisha
misaada kwa serikali ya Tanzania endapo ikiendelea kumfumbia macho bwana Jecha
kwa hatua yake ya kufuta uchaguzi
No comments
Post a Comment