WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AANZA KAZI NA MIKWARA KWA WATUMISHI,SOMA HAPO KUJUA
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa |
WAZIRU Mkuu wa
Tanzania, Majaliwa Kasim amewataka watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) kufanya kazi kwa weledi ili
kushughulikia matatizo yote yaliyotajwa katika hotuba ya Rais John Magufuli
wakati akizindua Bunge la 11. Anaandika Hamisi Mguta …
(endelea).
Waziri
Kasim amesema hayo leo jijini Dar es Salaam katika ziara yake kwenye Ofisi za
TAMISEMI kwa lengo la kuwakumbusha watendaji hao kuzingatia hotuba ya Rais
Magufuli.
Alifika katika ofisi
hizo mapema mchana na kufanya kikao cha faragha na watendaji wa ofisi hiyo
kilichochukua takriban dakika 45. Hata hivyo, alipotoka hakuwa tayari
kuzungumza na waandishi wa habari kwa wakati huo.
Akizungumza na
waandishi wa habari katika ofisi hizo, Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Jumanne
Abdallah amesema kuwa katika ziara hiyo Waziri Kasim amewataka watendaji
kufanya kazi kwa bidii na matunda yake yaonekane.
Amesema watumishi
hao wanapaswa kuwa na nakala ya hotuba ya Dk. Magufuli ili kujua mwelekeo
thabiti wa Serikali ya Awamu ya Tano.
Abdallah amesema
pamoja na serikali kujipanga kusaidia vijiji kimaendeleo pia uongozi wa vijiji
husika unatakiwa kujiwekea mikakati ya kimaendeleo ili kusaidia serikali katika
kutoa huduma hizo.
Amesema kuwa, kwa
uongozi wa mwaka huu jinsi ulivyojipanga, watendaji wa TAMISEMI wanapaswa
kufanya kazi kwa juhudu na kuwa mtu yeyote atakayelegalega katika kazi,
hatavumiliwa.
Kuhusu mgogoro
unaoendelea wa bomoabomoa, Abdallah amesema zoezi hilo linafanyika kuhakikisha
wanarudisha haki na kuwajibisha wanaotumia kigezo cha kuwa na fedha kujenga
katika maeneo ambayo si sahihi.
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni