KATIBU WA BUNGE AWAUMBUA WANAOJIFANYA WAPINGA POSHO,ASEMA WANALALAMA KWENYE MITANDAO TU LAKINI,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabweni miongoni mwa wabunge wanaolalamikia posho kupitia mitandaoni |
KATIBU wa Bunge
Dk.Thomas Kashilillah amesema kuwa, hadi sasa hajapokea barua ya mbunge yeyote
ya kukataa kupokea posho za vikao vya Bunge (Sitting alowances). Anaandika Dany Tibason, Dodoma …
(endelea).
Dk.
Kashilillah alitoa kauli hiyo wakati alipozungumza na mwanahalisionline mjini
hapa, kuhusu taarifa za baadhi ya wabunge kudai kukataa fedha hizo na baadala
yake zielekezwe kwenye shughuli za maendeleo ya jamii.
Ni siku moja tu
imepita baada ya Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu alidai kuiandikia
barua ofisi ya bunge kueleza kuwa, hatochukua posho hizo na badala yake
zielekezwe katika maendeleo ya jimbo.
Dk. Kashilila amesema, ofisi yake iko wazi, tayari kupokea barua
ya mbunge yoyote ambaye anakusudia kuandika barua ya aina hiyo kwa ajili ya
kufanyiwa kazi kulingana na maudhui hayo.
“Sisi tupo ofisini na hatujapokea barua yoyote, hatuwezi kufanya
kazi kwa kutumia magazeti au mitandao ya kijamii kwani kwa kufanya hivyo
tutakuwa tunakosea.
“Kama kuna mtu anataka asipokee hiyo posho, tutaona jinsi ya
kufanya lakini hatuwezi kumzuia mtu asifanye vile anavyotaka, ni matakwa ya mtu
mmoja mmoja,” amesema Dk. Kashilila.
Amesema iwapo mbunge ataandika basi itakuwa utashi wake mwenyewe
na si wa wengine “kwani wewe ofisini kwako ukisema hutaki kupokea mshahara,
watakulazimisha?, kwani wewe ukikataa mshahara na wengine watakataa” alihoji.
Mbunge mwingine ambayewahi kutangaza kutopokea posho hizo ni
Zitto Kabwe wakatia akiwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chadema.
Habari hii kwahisani ya mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni