WAZANZIBAR WAMTAKA ZITTO KABWE KUOMBA RADHI KWA RAIS SHEIN...
Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amepewa siku 14 kufuta kauli yake na kuomba radhi kwa kumhusisha rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na makosa ya uhaini.
Msimamo
huo ulitolewa na wagombea wawili wa nafasi ya urais wa Zanzibar, Juma
Ali Khatib (Tadea) na Soud Said Soud, walipokuwa wakizungumzia kauli ya
Zitto kudai haikuwa sahihi kwa Rais wa Zanzibar kubakia madarakani
wakati serikali yake imefikia ukomo wake Novemba 2, mwaka huu.
Soud
alisema kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar Kifungu cha 28 (1)(a), Rais
Shein ni Rais halali wa Zanzibar na atabakia madarakani hadi
atakapochaguliwa rais mpya kwenye uchaguzi wa marudio.
Alisema
kuwa Dk. Shein alichaguliwa na wananchi wa Zanzibar na haikuwa haki kwa
Zitto kumhusisha na makosa ya uhaini kwa kuendelea kubaki madarakani
kwani yuko kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
"Zitto Kabwe afute kauli yake na kuwaomba radhi wananchi wa Zanzibar ndani ya siku 14 na asipofanya hivyo tutamfungulia mashitaka." alisema Soud pia Mwenyekiti wa Chama cha AFP.
"Zitto Kabwe afute kauli yake na kuwaomba radhi wananchi wa Zanzibar ndani ya siku 14 na asipofanya hivyo tutamfungulia mashitaka." alisema Soud pia Mwenyekiti wa Chama cha AFP.
Katika
sakata hilo, Juma Ali Khatib, alisema tayari ameanza kutafuta namna ya
kuwasiliana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili
kuwasilisha malalamiko yake dhidi ya Zitto kwa kumhusisha na makosa ya
uhaini Rais wa Zanzibar.
Alisema
iwapo Bunge litashindwa kumchukulia hatua za kinidhamu Zitto, yeye
atalazimika kufungua kesi kwa niaba ya wananchi wa Zanzibar kupinga
kauli ya Zitto.
Khatib
alisema Zanzibar ni nchi na Rais wa Zanzibar lazima apewe heshima yake
kwa sababu kuendelea kuwepo kwake madarakani ni matakwa ya Kikatiba.
"Kumdhalilisha
Rais wa nchi ni sawa na kutudhalilisha wananchi wake, rais anashauriwa
na vyombo vingi vya sheria hivyo hawezi kuvunja Katiba," alisema Khatib
Viongozi
hao si wa kwanza kujitokeza kumtetea Rais wa Zanzibar kwani
walitanguliwa na aliyekuwa Kamishna wa Tume ya Rais ya Mabadiliko ya
Katiba, Simai Mohamed Said, tangu Zitto alipotoa kauli kuwa Zanzibar
haina rais na kuendelea kubakia madarakani Rais Shein ni sawa na kufanya
uhalifu wa uhaini.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni