Kleyah aachia video ya Msobe Msobe
MWANAMUZIKI KLEYAH AZINDUA VIDEO YAKE MPYA YA MZOBE MZOBE ALIYOMSHIRIKISHA BARNABA BOY
Mwanamuziki
wa Muziki wa kizazi kipya Maarufu kama bongo fleva KLEYAH ambaye
anakuja kwa kasi katika Tasnia hiyo hatimaye amezindua nyimbo yake mpya
inayokwenda kwa jina la MZOBE MZOBE wimbo aliomshirikisha msanii
maarufu maarufu kutoka THT Barnaba Boy CLASSIC nyimbo ambayo
inatabiriwa kufanya vizuri katika soko la musiki wa Tanzania.
KLEYAH
ambaye ni Mhitimu wa shahada ya mawasiliano kutoka chuo kikuu cha cha
Phoenix nchini marekani na baadae kufanya kazi katika shirika la
kimataifa la UNDP kabla ya kuacha na kuamua kurejea nchini kwa ajili ya
kuendeleza na kukuza sanaa yake Tayari amefanikiwa kufanya kazi na
watayarishaji na wasanii wakubwa ambapo mwaka 2014 alifanikiwa kufanya
nyimbo mbili ambazo zilirekodiwa nchini Kenya na mtayarishaji maarufu
nchini humo Lucas Bikedo pamoja na kufanyia Video kwa watayarishaji maarufu nchini Kenya kwa sasa OGOPA DJS.
Katika
nyimbo yake mpya ambayo ilizinduliwa Tarehe 6 Mwezi November na
kuchezwa katika vituo mbalimbali vya Radio nchini Tanzania na Africa
mashariki kwa ujumla na hatimaye leo umefanyika uzinduzi wa Video yake
ya wimbo wa MZOBE MZOOBE unataraji kutambulishwa katika vituo mbalimbali
vya Televission kwa ajili ya kumtambulisha msanii huyo ambaye
anaonekana kuja kwa kasi katika sanaa hii ya music wa kizazi kipya.
Akizungumza
nara Baada ya uzinduzi wa Video yake msanii KLEYAH amesema kuwa kwa
sasa mipango yake ni kuendelea kufanya kazi pamoja na watayarishaji
wakubwa nchini Tanzania pamoja na wasanii maarufu ili kukamilisha album
yake ambayo amepanga kuizindua mwezi July mwaka 2016 album ambayo
ametamba kuwa itasheheni aina mbalimbali za misic ili kuwafurahisha
mashabiki wanaofwatilia kazi zake.
Ameongeza
aliamua kufanya music kwa kuwa ni kitu ambacho kipo ndani ya moyo wake
huku akieleza kuwa kusoma na baadae kufanya music ni jambo la kuigwa na
wasanii wa Tanzania kwani itamsaidia msanii kutoboa tu si ndani ya nchi
lakini Barani Africa na duniani kwa ujumla
Hakuna maoni
Chapisha Maoni