ULINGO-UCHAGUZI HAUKUWA HURU NA WA HAKI,YASEMA KASORO LUKUKI,SOMA HAPO KUJUA
![]() |
Askari wakimshikiria mwananchi mmoja aliyedaiwa kufanya vurugu |
ULINGO – Taasisi
inayofanya kazi ya kuwajengea uwezo wanawake katika siasa, imesema uchaguzi
mkuu uliofanyika Oktoba 25 “haukuwa wa huru na haki kwa upande wa wagombea na
wapiga kura wanawake.).
Kauli
hiyo ya Ulingo imetolewa na Eva Maria Semakafu- Mratibu wa Ulingo, leo jijini
Dar es Salaam kwa waandishi wa habari, wakati taasisi hiyo ilipokutana na
waangalizi wa ndani kutoka mikoa 18, ambao walijikita kuangalia masuala ya
unyanyasaji na ukatili wa kijinsia kabla na wakati wa uchaguzi.
Semakafu amesema
“mara nyingi waangalizi wa uchaguzi hawatoi matokeo yanayohusu wanawake katika
uchaguzi…mwaka huu tumeamua kutuma waangalizi 56 wa ndani katika mikoa 18.
Hivyo tumebaini uchaguzi haukuwa wa huru na haki kwa sababu ya vitisho na
unyanyasaji waliofanyiwa wagombea na wapiga kura wanawake.”
“Sisi kwetu
wanaharakati tunasema, uchaguzi utakuwa wa huru na haki endapo wagombea na
wapiga kura wanawake watawekewa mazingira ya demokrsia bila ubaguzi hasa kwenye
vyama vya siasa,” amesema Semakafu.
Aidha, Shakira Mayamawa- mtafiti kutoka Ulingo ameutaja
unyanyasaji wa kijinsia uliojitokeza kabla na wakati wa uchaguzi kuwa ni;
wanawake kukataliwa na waume zao kuhudhuria katika kampeni, matumizi ya lugha
chafu dhidi ya wagombea wanawake na wanawake walioonekana kuunga mkono chama
fulani cha siasa kutoka kwa wanaume hasa vijana.
“Katika mchakato huu wa uchaguzi, nafasi ya ushiriki wa wanawake
imekuwa finyu. Katika kampeni za vyama vyote vya siasa, kwa kiasi kikubwa
wanawake walionekana ni wahamasishaji majukwaani. Hawakupewa nafasi ya kuwa
waongeaji kama ambavyo walipewa wanasiasa wanaume,” amesema Mayamawa.
Mayamawa amesema elimu inapaswa kutolewa ili kuondoa unyanyasaji
katika michakato ya uchaguzi. Vinginevyo changamoto hizo zinaweza kuzuia
ushiriki wa wanawake katika siasa.
No comments
Post a Comment