UCHAGUZI WA KATA YA SARANGA MANISPAA YA KINONDONI RASMI JUMAPILI,SOMA HAPO KUJUA
MANISPAA ya Kinondoni imewataka wakazi wa kata saranga ambayo haikufanya uchaguzi kwa ngazi
ya Diwani kujitokeza siku ya jumapili ya tarehe 15 mwezi huu kwa ajili ya
kupiga kura ili kumchagua diwani wanaomtaka.Anaandika KAROLI VINSENT endelea
nayo.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa Manispaa ya
Kinondoni Eng. Mussa Natty amesema taratibu za maandalizi ili kulekea siku ya
uchaguzi umekamilika kwa kuandaa vifaa vyote vya uchaguzi wa ngazi ya Udiwani,
Amesema
Uchaguzi huo ambaoulitarajiwa kufanyika Octoba 25 mwaka huu ulihairishwa
kutokana na kuwepo dosari kadhaa.
Amezitaja
Dosari hizo zilizopelekea uchaguzi kuhairishwa ni kutokea kwa vurugu kubwa siku
ya kupiga kura
“Mnamo saa 11 asubuhi siku hiyo ya tarehe 25 Octoba
ambayo ilikuwa ni siku ya kupiga kura baadhi ya wasimamizi na watu
wasiojulikana kufika katika eneo la
ugawajwi wa vifaa vya uchaguzi iliopo eneo la TANROAD Temboni”
Amesema baada hali hiyo kutokea ndipo baadhi ya
vifaaa vilipotea kutokana na vurugu hizo,
Sanjari na vurugu hizo Eng Natty ametaja kasoro
zengine ni kuwepo na upungufu wa karatasi
za kupigia kura jambo lilowafanya kuhailisha uchaguzi huo.
Hata hivyo Mkurugenzi huyo,amewataka wakazi ya kata
Saranga kujitokeza kwa wingi siku ya Jumapili ili waweze kumchagua Kiongozi wa
ngazi ya Diwani.
Ambapo amesema Manispaa yake imeafanya juhudi kubwa
ya kuwataharifu wakazi wa kata ya saranga kwa kutumia magari kutoa taarifa.
No comments
Post a Comment