SHEIKH PONDA AKWAMA TENA,AZIDI SOTEA KESI YAKE,SOMA HAPO KUJUA

MAHAKAMA ya hakimu mkazi Morogoro,kwa mara nyengine
tena imehairisha hukumu ya kesi Jinai inayomkabili kiongozi wa Taasisi ya Dini
ya Kiislam nchini ,Sheikh Ponda Issah Ponda.Anaandika KAROLI VINSENT endelea
nayo,
Kesi hiyo ilitarajiwa kutolewa hukumu leo Jumatano na Hakimu Makazi wa Mahakama
hiyo,Mery Moyo,imehairishwa na Mtuhumiwa amerejeshwa Rumande baada ya kuelezwa
hakimu kutokewepo Mahakamani kutokana na kwenda kwenye kozi fupi ya kusimamia
kesi za uchaguzi Mjini Dodoma.
Ambapo shauri hili limehairishwa hadi tarehe 30 ya
mwezi huu Novemba na Hamimu Mkazi ,Erick Rwechumbiza ambapo siku hiyo mtuhumiwa
atafikishwa mahakamani hapo.
Mshtakiwa huyo anakabiliwa na mashtaka mawili
ikiwemo kushawishi wa imani wa dini ya Kiislam nchini kutenda makosa,ambayo
anadaiwa kutenda kosa Ogost 2013,
Upande wa mashtaka uliwakilishwa na wakili wandamizi
wa Serikali Berdard Kongola,Sunday Hrela na George Mbalasa wakati wa upande wa
Mshtakiwa unawakilishwa Wakili Juma Nasoro ,Abubakal Salim na Bartholomeo
Tarimo.
Awali kesi hiyo ilipangwa kutolewa hukumu 19 ya
mwezi wa kumi ambapo shauri hilo lilihairishwa hadi Novemba 18 , ya leo,ambapo
tena limepigwa kalenda haki Novemba 30 ya mwezi huu,
No comments
Post a Comment