MAGUFULI KUKIONA SASA,UKAWA WAAPA KUFIA BUNGENI IJUMAA HII,TUNDU LISSU ASEMA PATACHIMBIKA MPAKA ZANZIBAR KIELEWEKE,SOMA HAPO KUJUA

Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa), umesema utakuja na stahili mpya wakati Rais Dk. John Magufuli,
atakapokwenda kuzindua na kuhutubia Bunge Novemba 20, mwaka huu.
Umesema staili watakayoitumia ni
tofauti na ile waliyoitumia wakati Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete,
alipozindua Bunge la 10 mwaka 2010 ya kutoka nje ya ukumbi kuonyesha kutotambua
serikali yake.
Akizungumza na mtandao huu katika
viwanja vya Bunge mjini Dodoma jana, aliyekuwa Mnadhimu wa Bunge la 10 Kambi la
Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, alisema safari hii hawatatoka nje ya ukumbi wa
Bunge hata kama hawamkubali Rais Magufuli, kwa kuwa ni wajibu wao
kushiriki vikao vya chombo hicho cha kuwakilisha wananchi.
“Sisi ni wabunge, tumo humu kwa
ridhaa ya wananchi, tuna haki ya kuingia bungeni, hivyo siku hiyo tutaingia
lakini kitakachotokea tutajua siku hiyo, bali haitakuwa kama walivyotuzoea
tunatoka nje,” alisema na kuongeza:
“Subira yavuta heri, bado siku tatu
tu, Watanzania watajua msimamo wetu tukiwa ndani ya Bunge nakuhakikishia lazima
pachimbike,” alisema.
Kuibuka huko kwa Tundu Lissu kuna kuja ikiwa ni baada ya taarifa kuzagaa mitandaoni zikisema ijumaa ya wiki hii Magufuli atalihutubia Bunge hili,huku inatajwa kuwepo na Rais aliyemaliza mda wake visiwani Zanziabr Dk Sheni jambo ambalo linatajwa ni uvunjavi wa katiba na kuna kwenda na kinyume na utawala bora.
Kwakuwa Ukomo wa Dk Sheni ulikoma
rasmi tarehe 2 ya mwezi huu kama katiba
inavyomtaka kwihiyo kitendo cha kuwepo madarakani hakikubaliki na kinatafsiriwa
ni sawa na udikteta.
Kuzidi kukaaa huko madarakani kwa
Dk sheni kunatokana na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi,Zanzibar ZEC,Jecha Salim
Jecha kufuta uchaguzi wote visiwani humo bila ya kupewa mamlaka yeyoet ya Katiba,Uchaguzi huo ambao Jecha alifuta inelezwa kuwa mgombea wa chama
cha wananchi CUF ambaye anaungwa mkono na UKAWA,Maalim Sefa sharif Hamad
kuibuka ushindi wa nafasi ya Urais
Hivi karibuni aliyekuwa mgombea
urais wa Ukawa kupitia Chadema, Edward Lowassa, alisema hawatambui matokeo
yaliyotangazwa na Tume yaTaifa ya Uchaguzi (Nec) na kumpa ushindi Rais Magufuli
na kwamba hawatashirikiana na serikali yake kutokana na kile alichoeleza kuwa
uchaguzi mkuu uligubikwa na wizi wa kura na kuporwa ushind
No comments
Post a Comment