SHEHE PONDA AIBWAGA SERIKALI MAHAKAMANI,APANGUA KESI ZOTE,SOMA HAPO KUJUA
Mahakama
ya hakimu mkazi Morogoro imemuachia huru Katibu wa Jumuiya na Taasisi za
Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda aliyekuwa akituhumiwa kwa makosa
ya uchochezi baada ya mahakama kutoridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka
na hivyo kuonekana hana hatia
Makosa yaliyokuwa yakimkabili ni mawili ambayo ni
kushawishi watu kutenda kosa, pamoja na kutoa matamshi yanayoumiza imani ya
dini nyingine.
Hakimu wa kesi hiyo Mary Moyo amesema ushahidi
uliotolewa na upande wa mashitaka haukujitosheleza hivyo mahakama hiyo
imemwachia huru na rufaa iko wazi endapo upande wa mashitaka hautaridhika na
hukumu hiyo.
Shehe
Ponda alikuwa anakabiliwa na mashtaka mawili ikiwemo kushawishi wa imani wa
dini ya Kiislam nchini kutenda makosa,ambayo anadaiwa kutenda kosa Ogost 2013,
Upande
wa wa Serikali katika kesi hiyo uliwakilishwa na wakili wandamizi wa Serikali
Berdard Kongola,Sunday Hrela na George Mbalasa wakati wa upande wa Mshtakiwa
unawakilishwa Wakili Juma Nasoro ,Abubakal Salim na Bartholomeo Tarimo.
Awali
kesi hiyo ilipangwa kutolewa hukumu 19 ya mwezi wa kumi ambapo shauri hilo
lilihairishwa hadi Novemba 18 na kuhairishwa tena mpaka kutolewa hukumu hiyo
leo,
Hakuna maoni
Chapisha Maoni