RAIS MAGUFULI KUMLIZA JOSEPH KUSAGA WA CLAUDS MEDIA,SUALA LA MATAMASHA LAZUA SINTOFAHAMU,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Rais John Magufuli |
MSIMAMO wa Serikali Rais John Magufuli kutangaza
kuyafuta Matamasha na Makongamano yanayoandaliwa na serikali kunatajwa kuiweka
kwenye Sintofahamu Kampuni ya Primetime promotion.Mtandao huu
umedokezwa.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Kampuni
ya Prime Time Promotion ambayo inamilikiwa na Mkurugenzi wa Clauds Media,Joseph Kusaga
,kampuni hiyo ambayo inatajwa kuwa ilikuwa
inapewa Tenda ya kuandaa matamasha mbali
mbali ndani ya Serikali.
Taaria za kuyafuta Matamasha ndani ya serikali kulitangazwa na Rais
Magufuli wakati analifungua Bunge juzi mjini Dodoma ambapo alitanga kwa kauli moja kuwa Serikali yake
itahakikisha inayafuta Matamasha,Makongamano pamoja na warsha ndani ya serikali
kwa kusema yalikuwa yanatumia pesa za bure huku akitazimia pesa hizo kuwa zitaelekezwa kwenye masuala ya maendeleo.
Kwa
mujibu wa Chanzo chetu cha kuaminika kilichopo ndani ya Serikali kimeuambia
mtandao huo kuwa endapo Rais Magufuli
akilitekeleza suala la kufuta matamasha na Makongamano basi kuna baadhi ya
kampuni yataumia.
“Yaani
nakuapia kabisa ndugu, ilo suala analosema Rais Magufuli la kufuta Matamasha
akilitekeleza kweli wataumia watu hapo,mmoja wao marafiki zangu wale mabosi wa clauds media na
kampuni yao ya primetime promotion(anawataja) pamoja na wale wa wasanii wa
(Tanzania house of Talent,THT) maana walikuwa wanapata kipato sana kupitia
matamasha mengi ya serikali”kimesema Chanzo hicho.
Kampuni ya
Prime Time promotion ambayo ni kampuni ya kiburudani na inakazi ya
kuandaa,maonyesho mbali mbali pamoja na kuwasimamia wasanii wakati wa
kutumbuiza kwenye matamasha mbali mbali,
Kampuni
hiyo licha ya kuandaa matamasha mengi pia ilikuwa inapata hata Tenda ya kuandaa
baadhi ya Matamasha ambayo serikali ilikuwa inaona uladhima wa kushirikisha
kampuni Binafsi.
Kutangaza
huko kwa Rais Magufuli kuyafuta matamasha hayo, kuna kuja ikiwa ni wiki tatu kupita baada ya Gazeti la
Mwanahalisi kuripoti kuwa Serikali iliyomaliza mda wake ya Rais Jakaya Kikwete
imemaliza pesa zote Hazina kutoka na matumizi ya anasa aliyokuwa anafanya Rais
Kikwete kwa Safari za nje na kuipelekea kuiacha nchi haina kitu.
Taarifa
ya Gazeti hilo ilikuja kuungwa mkono na Rais Magufuli Juzi alipokuwa analihutubia Bunge ambapo naye kwa masikitiko makubwa alisema safari za nje
zimelimaliza Taifa kifedha.
Hoja ya
Suala za Safari za nje, ziliwai ibuliwa na Mwenyekiti mwenza wa Vyama
vinavyounda,UKAWA,James Mbatia ambapo naye alisema safari hizo zimeliangamiza
Taifa kwakuwa zilikuwa hazina tija,
Ambapo wakati Mbatia analisema suala hilo,uliokuwa Utawala
wa awamu ya nne kwa kupitia kitengo cha Mawasiliano Ikulu ilibuka na kupinga
kwa nguvu zote huku wakisema safari hizo zinamanufaa.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni