MSIBA WA KAMANDA WA CHADEMA GEITA,UKAWA YATOA MCHANGO HUU KWA FAMILIYA YAKE,SOMA HAPO KUJUA
WABUNGE wa vyama
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wamepanga kuchanga Sh. 33.9
milioni kwa ajili ya kusaidia familia ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoani wa Geita, Alfonce Mawazo. Anaandika Dany Tibason … (endelea).
Fedha, hizo zimepatika baada ya wabunge 113 wa
Ukawa kuchangishana kiasi Sh. 300,000 kila mmoja ambazo zitakabidhiwa familia
ya Mawazo ambaye ameuawa kikatili na watu ambao mpaka sasa hawajabainishwa.
Mwenyekiti wa Chadema – Taifa ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa
Ukawa, Freeman Mbowe alisema hayo wakati akizungumza na mwanahalisionline mjini
hapa Dodoma kuhusu maandalizi ya mazishi ya kada huyo ambaye anatajwa
kuwa shujaa katika mapambado ya kutafuta ukombozi Ukawa.
Mbowe amesema licha ya kwamba Mawazo alikuwa mwanachama wa
Chadema lakini pia alishiriki vyema katika ukombozi ndani ya Ukawa kwa kutetea
masilahi ya Watanzania kwenye mkoa wake wa Geita pamoja na mikoa mingine
nchini.
“Kwa ujumla wetu wabunge takribani 113 tumekubaliana kuchanga
kiasi cha Sh. 300,000 kila mmoja kwa ajili ya kuiwezesha familia yake ambayo
ameiacha.
“Kumbuka kwamba Mawazo amepigania masilahi ya Watanzania wengi
katika mkoa wake wa Geita lakini pia katika maeneo mbalimbali ya Tanzania.
“Hivyo tunalazimika kumuenzi ikiwa ni pamoja na kuimarisha
ushirikiano wetu wa Ukawa na ikumbukwe kuwa, kwa sasa seriali ya CCM inaonesha
wazi kutumia vyombo vyake vya dola kudidimiza upinzani,” amesema Mbowe.
Hata hivyo, Mbowe amesema inasikitisha kuona jeshi la polisi
linavyotumiwa vibaya na kujikuta linafanya kazi za siasa badala ya kusimamia
ulinzi na usalama wa raia.
“Leo (juzi), baada ya viongozi wa Mji wa Mwanza kupambana vikali
na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, aliwaambia viongozi wa Chadema kuwa
intelejensia imeonesha kuwa, iwapo watafanya mkusanyiko wa ibada kuna uwezekano
wa kuzuka machafuko.
“Baada ya kupata taarifa hizo nilipata kuzungunza na IGP na
kuniahaidi kunipatia majibu lakini hadi sasa sijafanikiwa kupata majibu lakini
jambo lingine na la ajabu ni pale ambapo wamegeuza kibao na kusema hakuna
kufanya ibada kwani kwa sasa kuna ugonjwa wa kipindupindu hivyo hakuna
mkusanyiko,” amesema Mbowe.
Mbowe amesema lazima Watanzania watambue kuwa serikali inatumia
vibaya vyombo vyake vya dola kuzuia wapinzania wasifikishe ujumbe wao kwa
jamii, imekifia hatua ya kuzuia hata watu kuwazika wafuasi wao.
“Sasa angalia kutuuwa wanatuuwa lakini hatua ya kutunyanyasa na
kukataa hata tusimzike mtu wetu jambo hilo ni la ajabu sana lakini najua tutafikisha
ujumbe kwa njia nyingine ambayo inafaa na kwa ustaarabu,” amesema Mbowe
Hakuna maoni
Chapisha Maoni