POLISI YAMDAKA KIGOGO WA KAMPUNI YA BAKHARESA,NI WIZI WA KONTENA 329 BANDARINI,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
JESHI la Polisi nchini limethibitisha kumkamata Msimamizi mkuu wa kitengo cha ushuru wa forodha (ICD) kutoka kampuni ya Azam Eliaichi Mrema kutokana na upotevu wa Kontena 329 kwenye Bandari ya Dar es Salaam.
Hata Hivyo Jeshi hilo linawashirikilia watuhumiwa wengine kuhusu upotevu huo ambao ni Taigi Masamaki ambaye ni Kamishna wa idara ya forodha za ushuru kutoka Mamlaka ya Kodi nchini (TRA) na Habib Mponezia ambaye naye ni meneja wa kitengo cha ushuru wa TRA, na Hamis Ally Omary mchambuzi wa mwandamizi wa masuala ya biashara TRA.
Sanjari na hilo pia Jeshi la Polisi linawashirikilia watu wengine saba ambao hawakutaka kuwataja majina yao,
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini CP Diwani Athuman amesema mara baada ya Waziri mkuu Kassim Majaliwa kufanya ziara ya kushtukiza ijumaa ya wiki iliyopita Bandarini hapo aligundua kuna upotezi wa Kontena hizo na kuliagiza jeshi hilo kuwachukulia hatua watendaji waliohusika na upotevu huo,
“Waziri mkuu alipotuagiza kufanya uchunguzi,ndipo tukafanya uchunguzi kwa kushirikiana na watalamu waliobobea kwa kuchunguza masuala ya uharifu nchini na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa 12 ambao tumewatajieni watano harafu watuhumiwa wengine saba hatuta wataja kutokana na kutoharibu uchuguzi”amesema CP Athuman,
CP Athuman ameongeza kuwa watuhumiwa hao watafikisha Mahakamani mara moja baada ya kukamilika kabisa uchunguzi, huku akisema uchunguzi unazidi kuendelea kuwabaini wahusika wengine.
Vilevile CP Athuman amewashukuru Wananchi kwa ushirikiana walioutoa kwa kutoa taarifa kuhusu watuhumiwa hao.
Maoni 1
sasa tunadanganywa hapa ....yani hajui mchezo au wanamuogopa mkubwa...yale yale kudanganya watu...kamata bosi wa kampuni msitudanganye
Chapisha Maoni