MWENYEKITI WA ZEC AZIDI ZOMEWA,ACT WAZALENDO NAO WAMSHUKIA JECHA WAUNGANA NA CUF KUDAI HAKI,SOMA HAPO KUJUA

Vyama vya upinzania kisiwani Zanzibar vimetofautiana kuhusu
uamuzi wa mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha
kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa maelezo kuwa haukuwa huru na
haki.
Jana Chama Cha ACT-Wazalendo kiliunga mkono chama cha CUF,
kupinga uamuzi huo wa Mwenyekiti wa ZEC.
Akiongea na waandishi wa habari visiwani humo, Makamu mwenyekiti
wa ACT-Wazalendo, Ramadhani Suleiman alisema kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru na
haki kama ulivyoshuhudiwa na waangalizi wote wa ndani na nje ya nchi na kuitaka
Tume hiyo kuendelea na zoezi la kuhakiki matokeo na kumtangaza mshindi.
Wakati huohuo, vyama vya CCK, TLP na SAU wao kwa pamoja
walijitokeza na kuunga mkono uamuzi uliofanywa na mwenyekiti huyo wa ZEC
wakidai kuwa uchaguzi huo ulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa taratibu na kasoro
nyingi zilibainika hasa katika visiwa vya Pemba.
“Tunaunga mkono kauli iliyotolewa na mwenyekiti wa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi Zanzibar, ya kufuta matokeo ya uchaguzi huo kutokana na vikwazo
ambavyo Tume hiyo ilikabiliana navyo katika uendesha uchaguzi huo,” alisema mmoja kati ya wawakilishi wa vyama
hivyo.
Mwenyekiti wa ZEC alitangaza kufuta matokeo ya uchaguzi huo muda
mfupi baada ya mgombea wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kutangaza kuwa
amekusanya matokeo ya vituo vyote na kubaini kuwa yeye ndiye mshindi huku
akiitaka Tume hiyo kumtangaza.
Uchaguzi huo ulishuhudiwa kuwa na wagombea wa urais 14 lakini
wagombea wawili, Maalim Seif Sharif Hamad (CUF) na Rais wa sasa, Dkt. Ali Shein
(CCM) ndio waliokuwa na ushindani mkubwa zaidi.
Mpekuzi blog
a
No comments
Post a Comment