MAUZO KATIKA SOKO LA HISA YASHUKA KWA WIKI HII,SOMA HAPO KUJUA
Meneja Masoko wa DSE Patrick Mususa wakati wa mkutano na waandishi wa Habari akielezea hali ya mauzo katika soko la hisa |
IDADI ya Mauzo katika soko la hisa mkoani Dar es
Salaam,(DSE) kwa wiki hii yameshuka kwa asilimia kwa asilima 55% hadi Bilioni 12.5
kutoka Bilioni 28 kwa wiki iliyopita.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es
Salaam,Meneja Masoka wa DSE,Patrick Mususa amesema sababu iliyochangia kushuka
kwa mauzo hayo inatoka na wawekazaji kupunguza hisa zao katika kaunta ya TBL.
Mususa amesema pia
Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imepungua kwa asilimia 19% pia hadi
Milioni 1.7 kutoka Milioni 2.1 kwa wiki iliyopita.
Hata
hivyo Mususa amezitaja Kampuni tatu zilizoongoza kwa mauzo ya hisa ni . CRDB
kwa asilimia 47.88%2. TBL kwa asilimia 44.86%
pamoja na Benki ya DCB kwa asilimia 2.86%
Mususa amesema idadi ya mtaji katika soko
imeongezeka kwa wastani kutoka Trilioni 21 hadi Trilioni 21.1 pamoja na Idadi
ya mtaji wa makampuni ya ndani nayo imeongezeka kwa wastani kutoka Trilioni 9.7
hadi Trilioni 9.8,
Vilevile Mususa akawataka watanzani kuendelea
kununua hisa katika soko hilo kwa
kupitia huduma ya kisasa ya simu kwa kupiga *150*36#
No comments
Post a Comment