CHAMA KIPYA CHA SIASA CHAANZISHWA,SOMA HAPO KUJUA
MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA AKIKABIDHI CHETI KWA MMOJA WA WAANZILISHI WA CHAMA KIPYA CHA TPF MASHUJAA. |
MSAJILI wa
vyama vya Siasa nchini amekipa usajili chama kipya cha kisiasa cha Tanzania Patriotic Front (TPF Mashujaa).Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo
Akitoa usajili huo leo jijini Dar es Salaam Mbele ya Wanahabari,Msajili wa Vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi amesema amekipa usajili wa mda chama hicho mpaka pale kitakapokamilisha sifa za usajili.
Amezitaja Sifa hizo ni kupata idadi ya wanachama kutoka katika mikoa yote ya Tanzania bara pamoja na Visiwani.
Kwa upande wake Optatus Likwelile ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa chama hicho kipya, amewaambia wanahabari kuwa chama
chake kitasimamia misingi ya haki ya umoja pamoja na kupambana na umasikini.
No comments
Post a Comment