MALINZI AWAPONGEZA SAMATTA, ULIMWENGU
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi amewatumia
salamu za pongezi wachezaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu
wanaochezea klabu ya TP Mazembe ya Congo DR kufuatia kutwaa Ubingwa wa
Ligi ya Mabingwa Afrika (CL) jana kwa kuifunga timu ya USM Algiers kwa
jumla ya mabao 4-1.
Katika
salamu zake kwenda kwa wachezaji hao, Malinzi amewapa hongera kwa
mafanikio waliyofikia ya kutwaa ubingwa huo wa vilabu Afrika, na
kuwataka waongeze bidii ili waweze kufanya vizuri pia katika michuano ya
Kombe la Dunia la Mabara litakalofanyika mwezi Disemba nchini Japan.
Malinzi
amesema kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu na Watanzania wote
wanawashukuru kwa kuiwakilisha vizuri Tanzania kimataifa, na sasa moyo
huyo wa kujituma kwao waundeleleze katika mchezo dhidi ya Algeria
wikiendi hii kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la Dunia 2018 nchini
Urusi.
No comments
Post a Comment