Zinazobamba

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA JUU YAUFYATA ,YATOA MAJINA MENGINE,SOMA HAPO KUJUA


BODI  ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuutaarifu umma kuwa kuna taarifa zinazosambazwa na baadhi ya mitandao ya kijamii kuwa Bodi haitatoa
mikopo kwa waombaji wapya kwa mwaka wa masomo 2015/2016. Taarifa hizo si za kweli na hivyo Bodi inauomba umma kuzipuuza. 

Aidha, Bodi ya Mikopo inapenda kutoa taarifa kwamba hadi sasa imekwishawapangia mikopojumla ya waombaji mikopo wenye sifa 40,836wa mwaka wa kwanza. Katika awamu ya kwanza, Bodi ilitoa orodha yenye jumla ya waombaji 12,282 waliofanikiwa kupata mikopo na katika Awamu ya Pili iliyotolewa tarehe 9 Novemba, 2015 jumla ya waombaji
28,554 wamepangiwa mikopo.


Majina ya waombaji waliofanikiwa kupata mikopo kutoka katika awamu zote mbili
yanapatikana kupitia mtandao wa Bodi wa olas.heslb.go.tz
na tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz). Aidha, orodha hizo
pia zimetumwa vyuoni kwa ajili ya taratibu za usajili.


Lengo la Bodi ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wenye sifa kupata mikopo katika mwaka wa masomo 2015/2016, ambao ni 50,830, wanapata mikopo.

Aidha, Bodi inapenda kuwasihi waombaji wa mikopo kuwa watulivu wakati mchakato wa upangaji wa mikopo kwa wanafunzi wenye sifa unaendelea.

            

Imetolewa
na:

MKURUGENZI MTENDAJI

BODI YA
MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

No comments