WAANGALIZI WA UCHAGUZI WAZIDI MIMINIKA NCHINI,SASA EAC NAO WATOA WAANGALIZI WAO,SOMA HAPO KUJUA
JUMLA ya waangalizi wa Uchaguzi 72 kutoka ndani ya
Jumiya ya Afrika Mashariki wamewasili nchini kwa ajili ya kutazama Uchaguzi
mkuu unaotarajia kufanyika mwishoni mwa wiki hii.Anaandika KAROLI VINSENT
endelea nayo
Akiwakaribisha
waangalizi hao,Katibu mkuu wizara ya uhusiano wa Afrika Mashariki Joyce Mapunjo ambapo amesema
kujitokeza kwa waangalizi hao hapa nchini inatokana na uhusiano mzuri
ulijengeka kati ya Tanzania na nchi zinazounda Umoja huo.
Amesema Waangalizi hao wanatakiwa kufuata taratibu
za Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini NEC,huku wakiwa na jukumu moja tu la
kuangalia haki na kanuni za uchaguzi zinafuatwa,
Amebainisha kuwa waangalizi hao mara baada ya
Uchaguzi mkuu kumalizika watakuwa na kazi ya kutoa mtazamo wa uchaguzi.
Kwa upande wake kiongozi wa Waangalizi hao ambaye ni
Makamu wa Zamani wa Rais wa Kenya,Moody
Awori amesema wao wamekuja kuhakikisha uchaguzi mkuu unafutwa huku sheria
ikizingatiwa,
Amesema Waangalizi hao watazunguka nchi nzima ili
kutazamia uchaguzi huu kama haki inafuatwa.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni