KIKWETE AKUMBUSHWA KUTANGAZA MALI ZAKE BAADA YA KUNG'ATUKA MADARAKANI
Mkurugenzi
wa Idara ya Utetezi na Maboresho kutoka Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu (LHRC), Harold Sungusia, amemkumbusha Rais Jakaya Kikwete,
asiondoke kimyakimya bila kutangaza au kuorodhesha mali alizochuma
wakati akiwa madarakani.
“Rais
Kikwete alijaza fomu ya mali alizokuwa nazo Ofisi ya Rais, Sekretarieti
ya Maadili ya Viongozi wa Umma, lakini hakutangaza. Tunasubiri kuona
sasa baada ya kumaliza atatangaza mali aliyopata akiwa madarakani,” alisema.
Alisema
mwaka 1995, Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, alipoingia madarakani
alitangaza mali zake, lakini alipong’atuka, ‘alisahau’ kutangaza,
pengine ni kutokana na majukumu aliyokuwa nayo kitaifa sasa tunasubiri
kuona kwa Rais Kikwete,” alisema.
Kwa
mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13, 1995 na
kanuni zake, mwananchi anaweza kupata taarifa za mali za viongozi kwa
kufuata utaratibu uliopo, lakini baada ya kupata taarifa hizo,
haruhusiwi kuzitangaza au kuzichapisha kwenye vyombo vya habari.
Hoja
hiyo iliibuka katika semina ya mafunzo kwa washiriki 103 yaliyoandaliwa
na asasi ya HakiKazi Catalyst ya jijini hapa, kuhusu ‘Maadili ya
viongozi na watumishi wa umma katika usimamizi wa rasilimali: Ipi nafasi
ya wananchi kuhimiza na kuchochea uwajibikaji?’
Washiriki wa mafunzo hayo walikuwa ni maofisa watendaji wa kata, mitaa pamoja na wenyeviti wa mitaa na vijiji, wawakilishi wa vyama vya siasa, viongozi wa mila, wenyeviti wa ufuatiliaji wa rasilimali za jamii (Sedla) kutoka mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara.

Aliwafundisha
washiriki hao kuhusu misingi ya maadili ya viongozi wa umma kama vile
kufanya kazi kwa uaminifu na huruma, kujizuia na tamaa na kujiheshimu,
kujituma na kutekeleza majukumu kwa umahiri na kufanya kazi bila
upendeleo.
Misingi
mingine ni kutoa tamko la rasilimali na madeni, kuepuka mgongano wa
kimaslahi, suala ambalo ndilo limelifikisha taifa hapa lilipo na kuepuka
kupokea zawadi, fadhila au maslahi ya kiuchumi yaliyokatazwa.
Lengo la semina hiyo ilikuwa ni kuwawezesha wananchi kupata ufahamu mpana wa maadili ya viongozi wa umma na nafasi ya wananchi kuhimiza na kuchochea uwajibikaji.
Lengo la semina hiyo ilikuwa ni kuwawezesha wananchi kupata ufahamu mpana wa maadili ya viongozi wa umma na nafasi ya wananchi kuhimiza na kuchochea uwajibikaji.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni