Zinazobamba

CCM Kuzuia Wanafunzi Wa Vyuo Wanaosafirishwa Kupiga Kura



Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dodoma kimesema kuwa kimejipanga kuhakikisha wananchi ambao sio wakazi wa maeneo husika mkoani humo hawashiriki kuwachagua viongozi wasiowahusu.

Katibu Msaidizi wa CCM Mkoa wa Dodoma, Othman Dunga aliyasema hayo hivi karibuni alipoongea na waandishi wa habari mkoani humo, ambapo alieleza kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali waliojiandikisha katika mkoa huo lakini hawaishi maeneo hayo hawataruhusiwa kupiga kura kuwachagua wabunge na madiwani.

“Zipo taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Ukawa wameanzisha utaratibu wa kukodi magari kwa ajili ya kuwaleta wanafunzi ambao wamejiandisha hapa kwa ajili ya kupiga kura. Huu ni ushahidi tosha kwamba sio wakazi wa Dodoma,” alisema Dunga.

“CCM tumejipanga kuhakikisha hawapigi kura za kiongozi asiyewahusu, mawakala wetu watakabidhiwa orodha ya wakazi na wataisimamia hiyo,” Dunga ananukuliwa.

Kulikuwepo na taarifa zisizo rasmi kuwa kuna ‘wasamalia wema’ ambao wamejitolea kuhakikisha wanafunzi wa vyuo vikuu waliojiandikisha katika daftari la wapiga kura wakati wakiwa vyuoni na sasa wako majumbani, wanarudi katika maeneo waliyoandikishwa ili wapige kura. 
 
Kwa mujibu wa Dunga, huenda wanafunzi hao wakaambulia kupiga kura kumchagua rais pekee katika eneo walilojiandikishia walipokuwa wanasoma vyuoni hapo.

Maoni 2

Bila jina alisema ...

mimi ni mmoja wa wanachuo wa udom ambaye nilijiandikisha kupiga kura yangu makole-chadulu ambapo ndipo ninapopanga chumba changu ni mkazi halali wa makole-chadulu.sasa hivi nipo dar-es-salaam likizo ndefu ya chuo.nimeshitushwa na mkakati hatari na wa kihuni wa CCM kwamba nitakapokwenda dodoma kuwahi kupiga kura,ccm watanizuia mlangoni.kwa hiyo watanipokonya na hiki kitamblisho changu cha mpiga kura? siwaelewi.kwa maana nyingine kwa ccm dodoma ni ya wazawa wa dodoma pekee.ukazi wangu kwa mujibu wa ccm,hautambuliki kwa sababu tuu ni mwanachuo udom.naomba muyathamini maisha ya wajumbe wenu wa mashina mtakaowapeleka kulinda milango ya vituo.maisha bado wanayapenda na wana watoto,msiwafanye kafara. na ni wazi tunaona huu ni mkono mrefu wa tume ya taifa ya uchaguzi huyu ni KAILIMA WA CCM,tutajibu mapigo tena kwa kishindo cha kuwa historia.hebu mthubutu.

Bila jina alisema ...

waandishi karibuni dodoma mje mjionee senema ya kusimulia wengine.sasa hivi sisi wana udom tunaendelea kuitafakari kauli ya zuio la ccm-dodoma.huyu katibu wake othman dunga katumwa tuu aseme,tunatafuta cha taarifa na leo hii tunakwenda tume ya taifa ya uchaguzi makao makuu kumtafuta "CHANZO"