WAZIRI BERNARD MEMBE APATA MAPOKEZI MAKUBWA BUKOBA AZOA WADHAMINI
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe
(kushoto) akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na
wananchi waliofurika nje ya Ofisi ya CCM Mkoa wa Kagera mjini Bukoba
Juni 20.2015, alipokwenda kwa ajili ya kutafuta wadhamini wa kumdhamini
ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama
hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 500 mkoani humo.
Picha zote na John Badi
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe
(mbele mwenye miwani) akiongoza umati wa wanachama wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) na wananchi waliofika kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa
Bukoba mkoani Kagera Juni 20.2015 na kufanya matembezi kutoka uwanjani
hapo hadi katika Ofisi ya CCM Mkoa, alipokwenda kutafuta wadhamini ili
aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho,
ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 500 mkoani humo. Kushoto kwake
Ini Katibu mstaafu wa CCM mkoa Kagera, Faustine Kamaleki.
Msafara wa bodaboda ukiongozi
msafara wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge
wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (hayupo pichani) baada ya kuwasili
mjini Bukoba mkoani Kagera Juni 20.2015,kwa ajili ya kutafuta wadhamini
wa kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa
tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 500
mkoani humo.



No comments
Post a Comment