SUMAYE AMTINGISHA TENA KIKWETE NA CHAMA CHAKE,APIGA MKWALA WAKE TENA,SOMA HAPO KUUJUA
![]() |
Mawaziri Wakuu Wastaafu, Fredrick Sumaye (kulia) na Edward Lowassa wakifurahia jambo
WAZIRI Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye,
amekitahadhalisha Chama cha Mapinduzi (CCM), kuacha kuteua mgombea Urais, ambae
anatumia fedha kuwahonga wananchi ili wamchague katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba. Anaandika
Moses Mseti, Mwanza … (endelea).
Sumaye amesema endapo chama chake
kitamteua mgombea urais ambae ni mtoa rushwa na muabudu rushwa, atakihama chama
hicho na kwamba hatakubali kuona jina lake linakatwa kirahisi na akaendelea
kuvumilia.
Sumaye ametoa
kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Shinyanga,
ambamo amesema endapo atakatwa jina lake kiharari na mgombea kuteuliwa
ambae sio muabudu rushwa atakuwa tayari kusaidiana nae.
Amesema kuwa baadhi
ya wagombea waliotangaza kuwania urais kupitia chama hicho, wengine kanuni
haziwakubalibali bali wanasindikiza wenzao katika kinyang`anyiro hicho hivyo
ana imani ataibuka kidedea.
“Watia nia 34
waliotangaza mpaka sasa, wapo wengine ambao hawaitaji urais na wala kanuni za
chama chetu haziwakubali hao wanasindikiza wenzao, hao tayari wameishajitoa wenyewe
na siwafikirii”.amesisitiza Sumaye
Hata hivyo amesema
chama hicho kinapaswa kuteua mtu ambae ni msafi asiekuwa na kashfa yeyote
atakaesababisha chama hicho kushindwa kutwaa dola katika uchaguzi mkuu wa
Oktoba Mwaka huu.
Amesema umefika wakati wa CCM kutafakari na kuchuja watangaza nia
waliojitokeza hata wale ambao wanasindikiza wenzao katika safari hiyo, ili
kutoa mtu ambaeambae ana nia thabiti kuwatumikia wananchi.
Ameongeza uchaguzi huu utakuwa na vitimbwi na vituko
vya kila aina hivyo watanzania wanapaswa kuwa watulivu katika kufanikisha
kumpata kiongozi ambae ni bora na muadilifu.
Amesema vyama vya
siasa nchini vinapaswa kutoa maelekezo mazuri kwa wananchama na wafuasi wao ili
kuepusha vurugu zisizokuwa za lazima katika uchaguzi huo na nkutetea maslahi ya
umma.
“Siasa ni hoja
na wala siasa sio kutumia nguvu, nondo, risasi, rungu na panga ili kuingia
ikulu, hapana ni kutumia hoja nzuri na kuwaelimisha wafuasi katika kufanya
mambo ambayo ni mazuri,” amesema Waziri huyo wa zamani.
Kwa hisani
ya Mwanahalisi oli

No comments
Post a Comment