MWIGULU AMVUA NGUO KIKWETE,AICHANACHANA SERIKALI,SOMA HAPO KUJUA
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akitangaza nia |
MWIGULU Nchemba, Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi katika serikali
ya Rais Jakaya Kikwete amesema, ili serikali iweze kufufua viwanda vya nguo,
maguni na samaki, ni sharti wananchi wafunge mikanda. Anaripoti Dany Tibason kutoka Dodoma … (endelea).
Aidha, Mwigullu ambaye alikuwa naibu
katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara hadi wiki iliyopita
amesema, kuna haja ya kubadilisha sheria ya kupambana na rushwa ili kila
atakayepatikana na vitendo vya rushwa, afukuzwe kazi, afilisiwe pamoja na
kufungwa jera kwa kosa la kuhujumu uchumi.
Kauli ya Mwigulu inatafsiriwa na
wachambuzi wa kisiasa kuwa ni ya kutoridhishwa na hatua ya Serikali ya Rais
Jakaya Kikwete ambayo inadaiwa kuchukua hatua zisizokidhi katika kuwadhibiti
watuhumiwa na ufisadi.
Akizungumzia wakati wa kutangaza nia
yake ya kugombea urais, Mwigulu amesema, Watanzania wengi wanasumbuliwa na
umasikini, ukosefu wa ajira na kwamba yeye ndiye suluhisho la matatizo hayo.
Alirejea wimbo uleule ambao umeimbwa
na wanachama wengine wa CCM kuwa taifa linasumbuliwa na mambo mbalimbali ikiwa
ni pamoja na umasikini wa kipato, ukosefu wa ajira pamoja na ukesefu wa huduma
bora za kiafya.
Akizungumzia masuala ya rushwa alisema,
kuna matatizo makubwa katika kupambana na rushwa na kujigamba ikiwa atafanikiwa
kuingia madarakani, basi atamaliza tatizo hilo.
“Yeyote atakayebainika kupokea
au kutoa rushwa mtu huyo atachukuliwa hatua zaidi na kufukuzwa kazi. Tutamfunga na kwamba kosa hilo
litaangukia katika makosa ya uhujumu uchumi,” ameeleza.
Hata hivyo, Mwigullu ambaye ameingia
serikali katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja, hakueleza wapi alikopata
mabilioni ya shilingi anayodaiwa kuyatumia kukodisha vikundi vya hamasa na
kampeni.
Mbali na hilo, Mwigullu amesema, wapo
watu aliyodai wanaaminisha wananchi, kwamba “kuongoza nchi kunategemea uzoefu
au kufanya kazi serikalini kwa muda mrefu.”
Alisema kuwa kuwa kijana au mzee pekee
haina maana kuwa hiyo ndiyo sifa ya kuwa kiongzi.
“Inawezekana mtu akawa
amefanya kazi kwa muda mrefu serikalini, lakini akawa wa kwanza katika kulitia
taifa hasara,” ameeleza.
Alisema ifike hatua sasa siyo kila mtu
aweze kulitumikia taifa kwa ajili ya kutatua matatizo ya wananchi.
Kuhusu mgawanyo wa rasilimali za taifa,
mwanasiasa huyo ambaye amewahi kutuhumiwa kubambikizia wanasiasa wa upinzani
kesi za ugaidi ametetea uchimbaji wa gesi asilia na kwamba hakuna makosa
yaliyofanyika.
Alisema, “Kuna watu huko
wanalazimisha kusaini mikataba na sasa hao nao walijue haiwezekani tukawa
tunaletewa mafedha katika makaratasi na mengine yanaenda juu kwa juu hilo
haliwezekani.”
Amesema ni aibu kuwa kila mwaka
serikali inadaiwa Sh.100 bilioni kwa ajili ya huduma za afya lakini cha
ajabu ni kuwa fedha hizo hazipatikani na badala yake wananchi wanaambiwa
wagonjwa wanunue dawa wenywe.
Kuhusu mikopo kwa wanafunzi, Mwigullu
amesema, katika uongozi wake, hakuna sababu yoyote ya mwanafunzi mwenye sifa
kukosa mkopo.
Alisema bado zipo familia
nyingi ambazo zinakabiliwa na umasikini hivyo lazima kuna haja ya wanafunzi
kupata mikopo.
Akizungumzia juu ya kufanya
kazi kwa mazoea alisema kuwa wapo watendaji wengi ambao wanafanya kazi kwa
mazoea.
Kuhusu
Muungano
Alisema kuwa serikali ya awamu
ya tano lazima itaakikisha inasimamia muungano wa Tanzania Bara na Zanziba
sambamba na kuimarisha uchumi wao.
Alisema kuwa ni lazima
kuimarisha bandari salama,viwanda bora pamoja na kuimalisha ulinzi na salama.
Akizungumzia masuala ya
migogoro ya alisema kuwa ni lazima kuwa migogoro hiyo ikomeshwe na kuwepo
mpango mzuri wa matumizi bora ya ardhi.
Alisema kuwa amejitathimini na
kuhakikisha kuwa hatawavusha watanzania na kukomesha kufanya kwa
mazoea,kusimamia rasilimali na kuzingatia usawa ndipo kufanya kazi kwa vitendo
na wakati
Chanzo ni Mwanahalisi
oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni