Zinazobamba

MSIBA WA MUFTI SIMBA WAMLIZA RAIS KIKWETE,AMTOLEA MANENO HAYA,YASOME HAPO KWA KUBONYEZA HAPO


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametuma
salamu za rambirambi kwa Waislamu wote nchini na Baraza Kuu la Waislamu
Tanzania  (BAKWATA)) kufuatia kifo cha Sheikh Mkuu wa Tanzania  Mufti Sheikh  Issa Bin Shaaban Simba.

    Marehemu Mufti amefariki  leo 15/6/2015 asubuhi katika hospitali ya TMJ – DSM alipokuwa amelazwa akisumbuliwa
na ugonjwa wa sukari na shinikizo la damu (pressure).

      "Kifo kinaleta huzuni, hata hivyo Kifo hakizuiliki, hatuna budi kukikubali na ni wajibu wetu kumuombea
Sheikh Mkuu kwa Mola wetu ampe mapumziko ya milele". Rais Kikwete ametuma salamu hizo za rambirambi kupitia kwa
     Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es SalaaM Sheikh Alhadi Mussa Salum.


     Rais mesema na kueleza kuwa "Kamwe
mchango wake hautasahaulika katika jamii yote kwa Ujumla na hakika sote tutamkumbuka" 
ameongeza.





Marehemu alijiunga na BAKWATA mwaka
1968 na amekuwa mwalimu wa chuo katika mikoa mbalimbali ya Mwanza, Bukoba na
Mwaka 1970 alikuwa Shekhe wa Mkoa wa Shinyanga.
       Rais amemuelezea Marehemu Mufti kama
mwalimu katika jamii ambaye alikua na uzoefu wa hali ya juu na mwenye kupenda dini yake na kuitumia kwa manufaa ya jamii iliyomzunguka

"Amekua mwalimu imara na mtu wa kutumainiwa na kutegemewa katika uislamu na jamii kwa ujumla, hakika
tutamkumbuka siku zote' Rais Kikwete ameongeza.


Shekhe Issa Bin Shaaban Simba alikuwa
na uzoefu  mkubwa ndani ya BAKWATA na  aliwahi kukaimu nafasi ya
mufti kwa siku 90, baada ya kifo cha Mufti Hemed mwaka 2002.
        Baada ya hapo akasimamia mchakato wa uchaguzi
wa Mufti Mkuu na baadaye 2003 akachaguliwa kuwa Mufti Mkuu wa Tanzania.

    Mwenyezi Mungu ailaze roho yake
pahali pema Peponi, Amina.




Imetolewa na :

Premi Kibanga,

Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,

Ikulu-DSM

15 Juni, 2015

No comments