Zinazobamba

HABARI KUBWA LEO,KIKWETE AACHWA "MTUPU" NA WATIA NIA YA URAIS,WENGI WAJIGEUZA WAPINZANI WAISHAMBULIA SERIKALI YAKE ,SOMA HAPO KUJUA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete
pichani ni Rais Kikwete

MAKADA wa chama cha Mapinduzi CCM waliotangaza nia za kutaka Urais ndani ya Chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu wa hapo baadae mwaka huu,wamemuweka “mtupu kama asiyekuwa na nguo” Rais Jakaya Kikwete.mtandao  huu unaweza Kuripoti,Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
       Makada hao ambao asilimia kubwa walikuwepo kwenye Utawala wa Rais Kikwete,wameonesha wazi kwamba kama hawakuwa nchini,kutokana na kuweka sera zao wakati walitakiwa hata kuzitelekeza  wakati wakiwa kwenye Uongozi.
       Miongozi mwa makada hao ni Waziri mkuu aliyejiuzulu kwenye kashfa ya Ufisadi kwenye Kampuni Tata ya Richmound , Edward lowassa ambaye aliwaambia watu wanaojiita “Jukwaa la Wahariri” wiki mbili zilizopita na kuponda sera ya Kilimo kwanza na kusema Elimu ndio ingetakiwa kuwa kipaumbele.
     Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli ni miongoni mwa watu waliitengeneza Ilani ya CCM mwaka 2005 wakati wa Rais Kikwete anaingia madarakani ,ambayo sera ya kilimo kwanza ndio ilikuwa miongoni mwa Ilani hiyo.
      Mbali na Lowassa makada wengine walioivua “nguo” Serikali ya Rais Kikwete ni Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba ambaye naye wakati akitangaza nia ya kutaka Urais ndai ya chama hicho kinachozeekea madarakani kwa kusema atapambana kuinua uchumi wa nchi huku akisema tangu apata Unaibu Waziri ameshudia misamaa ya kodi kwa matajiri.
Mwigulu ambaye alikuwa Naibu Katibu mkuu Bara CCM,ameonyesha kuwashangaza watu kwakuwa yeye alikuwa miongoni mwa Baraza la Mawaziri la Serikali ya Kikwete ambao kila jambo ambalo Serikali wanaamua lazima likubalike na baraza hilo lakini ameshindwa kupambana na suala hilo .
          Sanjari na Mwigulu Nchemba makada wengine walioiweka Rehani CCM ni Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika Steven Wassira ambaye naye alikemea Ufisadi ambayo chama chake kwa kiasi Kikubwa kimechangia kuleta Ufisadi huo.
       Naye Pia Waziri wa Uchukuzi Samwel Sitta naye wakati anatangaza nia Jimboni kwake alisema atahakikisha kudumisha muungano na kupambana na Rushwa na Ufisadi, wakati Sitta huyo ndio alikuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba ambalo kwa kiasi Kikubwa “lilizika” maoni ya Wananchi yaliyowabana wala Rushwa.
       Akizungumza na Mtandao huu Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM kutoka Mkoani Morogoro amesema kwa sasa CCM inavuliwa nguo.
         “Mimi nashangaa sana,hawa wote tu walikuwa kwenye utawala huu ambao Rushwa imekuwa kubwa,tena watuhumiwa wa Ufisadi wameachwa,harafu leo wanakuja kutuambia kwamba watapambana na Rushwa huu ni utoto tu wanamuabisha Mwenyekiti wetu”amesema mjumbe huyo
“Hawa watu wakati wakichangia Bungeni wanasema Serikali ya CCM,imefanya Makubwa,huku Serikali hiyo hiyo imekumbatia watu walioifilisi nchi kwenye Mikataba ya Richmound,mimi nawaomba watanzania tuwe makini jamani”amesema Wananchi wa kawaida.



Hakuna maoni