HABARI KUBWA LEO-MTIFUANO MKUBWA KWA MNYIKA,SAMSON MWIGAMBA AJITOSA,SOMA HAPO KUJUA ZAIDI
pichani ni Samson Mwigamba picha na Maktaba |
KILE
kinachoonekana ni kama Chama Kipya cha Siasa nchini cha ACT-Wazalendo
wamejipanga kumwondosha Mbunge wa Jimbo la Ubungo CHADEMA John Mnyika kwenye Ramani ya kisiasa nchini baada
ya Uchaguzi Mkuu hapo baadae mwaka huu zimebainika,Anaripoti KAROLI VINSENT
endelea nayo.
Baada ya
hivi sasa Katibu mkuu Taifa wa ACT-wazalendo Samsoni Mwigambakutangaza rasmi
kuwania Ubunge kwenye Jimbo la Ubungo
ambalo linashikiliwa kwa sasa na Naibu huyo Katibu Mkuu Chadema bara .
Mwigamba ameyasema hayo leo jijini Dar
es Salaam wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa Mtandao huu ambapo Mwigamba akusita kuzungumzia safari
yake ya kisiasa katika Uchaguzi mkuu ujao kwa kusema atagombea Rasmi Ubunge
kwenye Jimbo la Ubungo.
Kwa Mujibu wa Mwigamba anasema Sababu ya
kwenda kwenye Jimbo hilo inatokana na Mbunge wa sasa aliyopo kushindwa
kuwatendea haki wananchi wajimbo hilo ikiwemo kuwatimizia mahitaji muhimu.
“Nakuhakishia
Mwandishi nawania Ubunge kwenye Jimbo la Ubunge maana Mnyika ameshindwa kutimizia
Mahitaji muhimu wananchi wa Ubungo,mimi mwenyewe ni Mkazi wa Ubungo tunapata
tabu,leo Mbunge wetu yupo kwenye Kazi ya kukijenga chama chake cha Chadema
kuliko wananchi tuliomchagua sasa mimi najitosa rasmi nakuhakishia namtoa
mnyika”amema Mwigamba.
Mwigamba ambaye kabla ya kuhamia
ACT-Wazalendo alikuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Arusha na alifukuzwa kwenye
Chama hicho kikubwa cha Upinzania nchini kwa madai ya kuandaa Mipango ya
kumpindua Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe kwa kushirikiana na wenzake
ambaye ni Zitto Kabwe pamoja na Profesa Kitila Mkumbo ambapo-
Mwigamba alizitaja ahadi ambazo Mbunge Mnyika
alizihaidi mwaka 2010 kwa mujibu wa
Mwigama anadai ameshindwa kuzitimiza, ni
mahitajia ya Maji safi na salama ambayo
anadai limekuwa Tatizo kubwa kwa
wananchi wa Jimbo hilo pamoja na tatizo la usafiri ambalo anasema
ataweza kuliondoa kwa mda mfupi tu pindi atakapopata Ubunge huo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni