Zinazobamba

WAMILIKI WA MABASI WAIANGUKIA SUMATRA,PIA WAFICHUA SIRI ZA SABABU YA AJALI,SOMA HAPA KUJUA

CHAMA cha Wamiliki wa Mabasi  nchini (TABOA) wameitaka Mamlaka ya Usafirishaji wa  Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kuwapa miezi mitatu ya Majaribio ili kutekeleza Azamio la Mamlaka hiyo linalowataka wamiliki hao kuwaajiri madereva wawili kwenye mabasi yanayokwenda masafa marefu.Anaripoti KAROLI VINSENT endelea nayo 
         Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa (TABOA)Elenea Mrutu wakati wa mkutano mkuu wa Dharula uliowakutanisha wamiliki mbali mbali wa Mabasi wenye lengo la kujadili wimbi la uongezeko la Ajali linaloongezeka kila kukicha nchini.
       Ambapo amesema nia ya Serikali na Sumatra kuwataka wamiliki hao kuwa na utaratibu wa madereva wawili ni nzuri ila wanaitaka mamlaka hiyo kutoa miezi mitatu ya maribio ili kuweza kujua umuhimu wake na kujiweka utayari wa kutekeleza azimio hilo.
        Bwana Mrutu ameongeza kuwa kwa sasa Mfumo wa sasa wa kuwa na Dereva mmoja umesababisha madereva kuchoka na kupelekea kutokea kwa ajali ambapo amedai mfumo huu wa sasa wa kuwa na Madereva wawili utasaidia kuondoa Tatizo hilo ambalo limegalimu vifo vya Watanzania.
          Kwa upande wa Wamiliki wa mbalimbali wa Mabasi wameitupia lawama serikali kwa kushindwa kutekeleza matakwa yao ambayo walikuwa wanaitaka serikali kuongeza mda wa usafirishaji toka mda wa sasa wa saa kumi na mbili hadi masaa 24 jambo ambalo wanadai kufanya hivyo kutaweza kuwafanya madereva kupunguza mwendo kasi.

     Sanjari na hilo Wamiliki hao wamelalamikia pia Ubovu wa Miundombinu ikiwemo Barabara na msongamo usio na lazima ambapo bwana Emmanuel Sawaya Mmiliki wa Basi la Kilimanjaro Express anadai limesababisha Janga la Ajari nchini. 

No comments