HABARI KUBWA-GAZETI LA MWANANCHI LABOMOLEWA TENA,MHARIRI WAKE MWENGINE ACHUKULIWA,NI MUNDELEZO WA KUKIMBIWA SOMA HAPA KUJUA
| pichani ni Neville Meena picha na Maktaba |
NA KAROLI
VINSENT
ZIMWI la
kukimbwiwa na Waharri pamoja na Waandishi wake bora lazidi kulitesa Gazeti la Mwananchi baada
ya hivi sasa Mhariri wake Mwingine ambaye pia ni Msimamizi wa dawati la Habari za
Uchunguzi Neville Meena naye amelikimbia
Gazeti hilo na kuhamia Gazeti la kila
siku la Tanzania Daima.MTANDAO huu umedeokezwa.
Kuhama
huko kwa Neville Meena kumekuja ikiwa miezi michache kupita baada ya aliyekuwa
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi Tido Mhando kuhamia Kampuni ya
Azam media.
Taarifa za kuaminika ambazo mtandao huu umezipata
zinasema Neville Meena amehamia rasmi Gazeti la Tanzania Daima na kupewa nafasi
ya Mhariri Mtendaji.
Nafasi
ya mhariri mtendaji kwenye Gazeti hilo hapo awali ilikuwa inashikiriwa na Asbert
Ngurumo ambaye sasa amejiingiza katika masula ya siasa ambapo anatarajiwa
kugombea Ubunge kwenye Jimbo moja katika mikoa ya Kanda ya ziwa.
Neville Meena ambaye ni katibu Mkuu
wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEC) kuja kwake kwenye gazeti la Tanzania Daima
kunatajwa na wachambuzi wa Masuala ya habari ni kuzidi kuleta mapinduzi katika
Gazeti hilo bora kwa sasa nchini ambalo mara kwa mra limekuwa likimbumbana
vikwanzo na Serikali kutokana na kuchapisha habari Zenye kuihuzi idara
mbalimbali za Umma ambazo hazitaki kuambiwa ukweli.
Hii si mara ya Kwanza kwa Gazeti la
mwananchi kuzidi kukimbiwa na Wafanyakazi kwani kipindi cha Miaka miwili
iliyopita iliwai kukimbia na Wahariri wake ,waandishi pamoja wasambazaji wa
Gazeti hilo.
Wahariri hao ni Dennicy Msack ambaye nae
alikacha gazeti hilo na kumbilia kwenye Kampuni ya Newhabari ambao ni wachapishaji wa magazeti
ya Mtanzania,The African,Rai Nguvu ya Hoja,Bingwa pamoja Dimba.
Mbali na Msack wengine waliokimbilia
Kampuni ya NewHabari ni Edwin Mjahuzi ambaye alikuwa mpiga picha mkuu anatajwa
kuwa alikuwa kiungo muhimu kwenye gazeti la Mwananchi na mhariri wa Habari wa
Habari Samsoni Mfalila.
Si wahariri pamoja na wasambazaji tu
peke yake waliokimbia katika Gazeti la Mwananchi na hata wapiga picha
walikimbia Gazeti hilo na kwenda katika Gazeti la Mtanzania ambao ni Fedilis
Felix ambaye amepewa mataba nono wa kupiga picha kwenye Kampuni hiyo.
Kampuni ya Newhabari ambao inamilikiwa
na Bilionea Rostam Azizi pia ilizidi kulibomoa Gazeti la Mwananchi baada ya
kuendelea kuwachukua watu wake muhimu ambaye mwengine ni Msambazaji Msaidizi
Erasto Matasia.
Kukimbia huko kwa mwananchi
kunatafsiriwa tofauti na wachambuzi wa masula ya Habari kwamba Gazeti hilo
linapitia katika kipindi kigumu na linaitaji busara tu katika kukabiliana na hali hiyo.
Akilizungumzia hali hiyo ndani ya
Gazeti la mwananchi Msomi na mchambuzi wa
Masuala ya Habari kutoka chuo Kikuu Huria cha Tanzania Bilal soud alisema kwa
sasa gazeti hilo limekumbana pigo kubwa sana na dalili zimeonekana baada ya
maudhui ya Gazeti hilo kuwa tofauti na kipindi cha nyuma.
“Kusema
ukweli bila hata kuuliza kama Meena yupo au Tido utajua tu watu hawa hawapo
kwasababu Habari wanazozichapisha sahivi zimekuwa na zikionyesha kwamba gazeti
limekosa watu makini kama wakina Tido na wasipotafuta ufumbuzi wanaweza wakawa
sehemu sio nzuri”alisema Bilal
No comments
Post a Comment