Nimemsikiliza Mhe Rais. Ninachoweza
kusema ni kwamba maazimio yale hayakuwa ya
Zitto Kabwe, PAC, CAG au PCCB. Yalikuwa ni
maamuzi ya Bunge zima. Bunge la vyama vyote
kikiwamo chama cha Rais Kikwete yaani CCM.
Sisi kama Bunge tulitoa maazimio yale kwa
maridhiano, uzalendo na bila kutaka kumuonea
mtu yeyote. Suala hili sasa naliacha kwa
wananchi. Bunge limefanya kazi yake na Serikali
ambayo ndiyo tulikuwa tunasubiri maamuzi yake
imeamua hivyo. Wananchi wataamua wenyewe.