Zinazobamba

TGNP:TUMESIKITISHWA NA KIPIGO CHA WARIOBA, WAWA TAKA WANAWAKE WAJITOKEZE KUGOMBEA SERIIKALI ZA MITAA



Mtandao wa kutetea haki za kijinsia umetoa yake ya moyoni kuhusu tukio ambalo liliushangaza umma wa Kitanzania kwa kipigo ambacho alipata kiongozi mwenye sifa kemkem katika taifa hili, Mh. Jaji Joseph Sinde Warioba kwa kusema kuwa wamesikitishwa sana na tukio hilo na kulilaani vikali wakisema ni kitendo cha aibu ambacho waziri huyo mstaafu amefanyiwa katika taifa lake,

Akizungumza na Mtandao huu mapema hii leo,Mkurugenzi wa Idara ya Maarifa/Elimu, Utafiti na Uchambuzi Bi. Gloria Shechambo amesema tukio hilo ni la kulaaniwa kwa watanzania yeyote mwenye nia njema na taifa hili,

Shechembo ameenda mbele zaidi na kusema ule ni ukatili wa wazi kabisa ambao umeonyshwa kwa kiongozi huyo kupigwa hivyo ni wazi kabisa kwa mtanzania wa hali ya chini hatakuwa na uwezo wa kuthubutu kutoa yake ya moyoni kuhusu katiba mpya inayopendekezwa, 


Ukatili ule ulionyeshwa na genge la watu wachache limetuhudhunisha sana, na tunadhani sasa hata mwanamke huenda akaanza kuogopa kusema kwa kuhofiakupigwa na watu ambao wapo katika kusanyiko

Aidha katika hatua nyingine, Bi. Groli amewataka wanawake kuthubu kwa kujitokeza kugombea ili waweze kupendekezwa nakuchaguliwa katika uchaguzi wa serikali zamitaa unaotarajiwa kufanyika desember 14

Lazima wanawake tujitokeze tuachane na tabia ya woga kwani kukaa nyuma nyuma ndiko kunasabishwa tubaki nyuma siku zote aliongeza Bi grolia Shechambo.

Hakuna maoni