HABARI KUBWA LEO--MADUDU YA MAKONDA YAFICHUKA,ELIMU YAKE YAIBUA MAKUBWA KWENYE CHETI CHAKE,SOMA HAPA KUJUA
Na
Karoli Vinsent
HUKI ikiwa
bado wasomi,wanasiasa na wanaharaki pamoja na taasisi mbalimbali zikiwa zinalahani
vikali kitendo cha wahuni waliokodiwa na aliyekuwa Mjumbe wa Bunge Maalum la
katiba Paul monda kuvuruga na kumpigwa aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya
ukusanyaji Maoni ya Katiba mpya Jaji Joseph Warioba wakati mdahalo wa kutoa elimu kuhusu katiba iliyopendekezwa na Bunge maalum la katiba,sasa Mapya
yaibuka kuhusu Fujo hizo,Mtandao huu unariboti
Taarifa za kuaminika ambazo Mwandishi
wa Mtandao huu amezipata zinasema Chama cha Mapinduzi CCM kilikuwa nyuma za
vurugu hizo zilizoibuka wakati wa mdahalo huo wa kutoa elimu kuhusu katiba,na
kiongozi wa vurugu hizo ametajwa kuwa ni Paul makonda katibu wa uhamisishaji wa
umoja wa Vijana (UV-CCM),
Chanzo hicho kinasema Makonda
mabaye anadaiwa kukodisha vijana na kuwapa posho ili kuandika mabango
,kuyaingiza ukumbini na kutoa taarifa lini wanayanyue mabango yao ili kupoteza Mwelekea ukumbini hapo,
Na ndivyo ilivyotokea ukumbini
hapo siku ya jumapili wakati wa kungamano hilo Ubungo Plaza Jijini Dar Es
Salaam,
Makonda ambaye nyaraka mbalimbali
zinamuonyesha akitumia Jina Paulo Christian Makonda kutoka Wilayani
Sumve,Mkoani Mwanza.
Taarifa hizo kutoka kwa watu waliokaribu na Makonda zinasema kiongozi huyo wa UV-CCM alimlipa
kila kijana aliyefanya vurugu kiasi cha fedha cha sh 50,000(elfu Hamsini)
Taarifa hiyo ilizidi kusema mkutano wa Makonda kupanga njama za kuvuruga
mdahalo huo,ulifanyika siku Jumamosi ambapo kabla ya siku moja kufanyika kwa
mdahalo yaani siku ya jumapili na mkutano huo ulifanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam,
Ambapo mbali na Makonda kada mwingine aliyeshiriki katika uhujuma hiyo
alikuwa ni Salum Hapi ambaye ni katibu wa Zamani wa CCM katika vyuo vikuu vya
Mashariki na pwani ambaye sasa yupo makao makuu ya UV-CCM akisubili kupewa
uongozi.
Makonda ambaye ni Kijana anayetumiwa
na Msaka urais Samwel Sitta ,ndiye alikuwepo katika mipango ya kuanzisha chama cha Jamii CCJ.
Vyanzo mbalimbali vinamtaja Makonda
ambaye alikuwa anatumwa na Samwel Sitta kwenda
kwa Dk Wilbroad Slaa,katibu mkuu wa Chadema katika mpango wake wakuhamia
chama hicho kikubwa cha Upinzani nchini.
Mtandao huu umedokezwa Jina la
Christian ambalo Makonda anatumia kwa
miaka mingi sio la kwake halisi,inadaiwa
alijipachika jina hilo baada ya kufeli masomo yake ya Sekondari.
Ambapo Mwenye Jina hilo hasa ni Paul
Christian ni Mwandishi wa Habari ambaye anafanya kazi redio ya Kijamii Mkoani
Tabora.
Ujumbe wa simu ulionaswa na Mtandao
huu,unaonyesha wazi kwamba Paul Makonda ndiye aliyepanga mikakati hiyo ya
kuvuruga amani ukumbini hapo,
“Tuliitwa
jana (Jumamosi) na Makonda tukapewa
malekezo kuwa twende Ubungo plaza kuvuruga mdahalo ,tulikuwa ma kikundi cha
watu 25 hadi 30 ila leo tulifika watu 15
“ unaleza ujumbe mmoja wa simu
Ujumbe huu mwengine ulitumwa na kigogo wa chama cha Mapinduzi
CCM saa 11.39 jioni muda mfupi baada ya
mdahalo kuhailishwa ulisema hivi
“Wengine
hawakutokea kwasababu nadhani waliogopa ingawa posho ndogo walichukua,tulifika
ukumbini wakati mdahalo ushaanza”
Kwa Upande wake mwenyekiti wa Chama
cha wananchi CUF Profesa Ibahimu Lipumba
alilani vikali uhuni huo aliofanya Makonda wakati wa Mkutano na Waandishi
Wahabari juzi jijini Dar es Salaam,alisema kitendo alichofanya makonda kinafaa
kulaniwa na kila mtu.
Nao Asasi
mbalimbali za kiraia zimelaani vikali kitendo cha kipuuzi alichofanyiwa Jaji
warioba, Akisoma tamko la asasi hizo za kiraia kwa waandishi wa habari juzi
Jijini Dar es Salaam, Msomaji wa tamko hilo Bi Hellen
Kijjo Bisimba Ameweka wazi kuwa tukio la kupigwa kwa warioba lilipangwa na
genge la watu wachache ambao walikuwa na nia ovu ya kuharibu mkutano huo abao
ulilenga kutoa elimu kwa wapiga kura,
Aidha asasi hizo ambazo zilikuwa zikiongea kwa uchungu kutokana na kupigwa kwa Warioba, Wameionya vyombo vya dola kuhakikisha kuwa huo unakuwa ni mara ya mwanzo na ya mwisho kutokea kwa vurugu kama hizo kwani kitendo cha kuachilia hali kamahiyo kuendelea kutokea kutalipelekea taifa katika vita dhito amabayo itagharimu maisha ya awatanzania wote
Habari hii imeandikwa na mwandishi wa mtandao huu karoli Vinsent na kusaidiwa na Gazeti la mawio kwa baadha ya data
Aidha asasi hizo ambazo zilikuwa zikiongea kwa uchungu kutokana na kupigwa kwa Warioba, Wameionya vyombo vya dola kuhakikisha kuwa huo unakuwa ni mara ya mwanzo na ya mwisho kutokea kwa vurugu kama hizo kwani kitendo cha kuachilia hali kamahiyo kuendelea kutokea kutalipelekea taifa katika vita dhito amabayo itagharimu maisha ya awatanzania wote
Habari hii imeandikwa na mwandishi wa mtandao huu karoli Vinsent na kusaidiwa na Gazeti la mawio kwa baadha ya data
Hakuna maoni
Chapisha Maoni